28/04/2024
AYLF-UDSM Chapter, leo tumekutana katika Small meeting gathering ya mwisho kwa mwezi April na tulikuwa na Theme(mada) inayoitwa "RELATIONSHIPS AND RECONCILIATION". Mwl wetu wa leo alikuwa anaitwa WITNESSRUSSIA.
Alitukumbusha kuwa kiongozi mzuri ni yule anayejua na kutambua uhusiano wake yeye na MUNGU,familia na watu wengine wanao mzunguka.
Pia alitukumbusha kuyatambua maeneo muhumu katika maisha yetu yanayoitaji upatanisho kati yetu na MUNGU,familia na watu wanao tuzunguka.
Lakini aligusia njia na hatua muhimu zinazoweza kutumia kujenga uhusiano na upatanisho katika maisha yetu.
Alisisitiza jambo la muhimu zaidi kwetu sisi k**a vijana na viongozi wajao tunatakiwa kufwata na kuiga mfano na maisha ya YESU WA NAZARETH ambaye alifundsha upendo/mahusiano mazuri pamoja na kufanya upatanisho.hivyo njia pekee ya kuiponya jamii ni kujifunza KUSAMEHE. Alisema msamaha na kufanya upatanisho ndiyo itakuthibitishi kutokufanya au kulipa kisasi.
Aligusia aina mbili za msamaha
1.Unilateral forgiveness,huu ni msamaha unao toa pasina kuitaji chochote kutoka kwa yule aliyekutendea jambo.
2.Bilateral forgiveness,huu ni msamaha unaotolewa kwa kuhusisha pande mbil za watu au makundi na kwa lengo la kupata malipo au fidia.
alitufundsha njia muhimu za kuweza kusamehe kwa urahis,mduara wa kusamehe Vs kutokusamehe.
Alihitimisha kwa kutufundsha njia sahihi za kujenga urafiki wa muda mrefu ambazo ni,
1.intentionality(kuwa na watu wachache mnaoendana kifikra)
2.long term commitment
3.self-sacrifice(kujinyima)
4.trust-worthiness(ukweli na uaminifu)
5.able to forgive (kuwa tayari kusamehe)
6.take time (wape muda unao wapenda)
7.be present (uwepo wako kila wanapo kuhitaji)
8.express appreciation(eleza kushukuru kwako kwa mambo muhimu wanayokufanyia au kufanya)
9.listen(sikiliza zaidi)
10.learn to communicate
"Tumejifunza kupaa k**a ndege, tumejifunza kuogelea k**a samaki ila tumeshindwa kujifunza kitu kidogo tu. Kuishi k**a ndugu."(Martin Luther King Jr)
Godson Kitomary,
Ass Cordinator,
AYLF-UDSM Chapter,
April 28,2024.