12/11/2023
GSM alipotoa mabilion ya hela kuwaomba la liga waje watushauri kuhusu muundo wa klabu alijua kuwa tunahitaji mfumo Thabiti wa uwajibikaji, na muuda sahihi wa uendeshaji klabu
Mfano leo makolo wana mgogoro hawajui wamsulubu nani, wapo wanaomsulubu Nyekiti na wapo wanaomtetea.
Unajiuliza wakati wa African League nani alitambulishwa k**a nyekiti? Je nan mkubwa kati ya nyekiti na mwenye bilion 20?
Yaan custodian wa asilima 51 alipelekwa kukaa VIP C ? Halafu leo mnafungwa mnahitaji majibu kutoka kwake?
Shida inayowatesa mfumo wa mali kauli ambayo huku kwetu hayo madudu hayapo. Sisi mwenye mamlaka ni Rais wa klabu.
Madunduka walienda kwenye uchaguzi wa kumchagua nyekiti huku wakiwa hawana akidi (idadi ya wapiga kura). Yaan kuna mpiga kura alijisajili siku hiyo hiyo akaenda kupiga kura siku hiyo hiyo.
Zoezi la uchaguzi lilifanyika gizani, hakuna camera wala nini. Sasa k**a hakukuwa na uwazi kwenye jambo nyeti k**a hili mnategemea uwajibikaji kweli?
Hapa ndipo unapokumbuka kauli ya Mzee Rage. Makolo kilichopinda sio kivuli ni mti.
Hapa ndipo tulipowaacha mbali sanaaaaa. Yule Uchebe aliwaambia hamkumwelewa, Sven akaongea kwa mafumbo hamjamwelewa. Haya sasa Robatinyo nae kawaambia mna safari ndefu.
Hivi mnadhan kubeba medal ya CAF ni jambo rahisi? Linahitaji mfumo thabiti wa utawala kabla ya kufikiria kuhusu ubora wa timu.
Tumewaacha mbali sanaaaaaaaaaaaaa