Modern football clubs.

Modern football clubs. Karibuni katika page hii Kwa habari muhimu,biashara mbalimbali na matangazo Always we trust in true and fact
(3)

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said, amesema mafanikio ya Serikali kat...
03/06/2026

Mbunge wa Baraza la Wawakilishi na Mwakilishi wa Jimbo la Tunguu, Simai Mohammed Said, amesema mafanikio ya Serikali katika ukusanyaji wa mapato yanaonyesha kuwa Tanzania ipo katika mwelekeo sahihi wa kiuchumi chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Akichangia mjadala wa Bajeti ya Wizara ya Fedha Bungeni leo Juni 2, 2026, Simai amesema TRA, hata hivyo, alisema bado kuna baadhi ya watu wanaokwamisha juhudi za maendeleo kwa maslahi binafsi, akidai kuwa mmoja wao ni mtu aliyemtaja kwa jina la "Yuda" ndani ya Serikali.

"Kosa la Rais Samia ni lipi? Kumuamini mtu? Kumbe ni Yuda. Yuda huyu amewasaliti ndugu zake mwenyewe, hata familia iliyomlea kisiasa haitaki kumuona. Hata huko nyuma aliwahi kuitwa mzigo, lakini leo mzigo huo tunao ndani ya Serikali," alisema Simai.

Aidha, Simai alidai kuwa mtu huyo amekuwa chanzo cha maumivu kwa watu mbalimbali, akiwemo viongozi wa kisiasa, watumishi wa umma na wafanyabiashara, huku akisema baadhi ya waliokuwa na mustakabali mzuri wa kisiasa walipoteza nafasi zao kutokana na ushawishi wake na wengine kuingia katika changamoto za kisaikolojia.
football clubs

Bei mpya za mafuta zimeanza kutumika leo Juni 3, 2026, huku petroli jijini Dar es Salaam ikiuzwa kwa Sh4,086 kwa lita ba...
03/06/2026

Bei mpya za mafuta zimeanza kutumika leo Juni 3, 2026, huku petroli jijini Dar es Salaam ikiuzwa kwa Sh4,086 kwa lita baada ya kushuka kutoka Sh4,115 mwezi Mei, wakati dizeli ikipanda hadi Sh4,333 kutoka Sh4,248 kwa lita.

Kwa mujibu wa bei kikomo za rejareja zilizotangazwa na EWURA, mafuta ya taa nayo sasa yanauzwa kwa Sh4,685 kwa lita kutoka Sh4,677 mwezi uliopita.

EWURA imesema mabadiliko hayo yamechangiwa na kuongezeka kwa gharama za mafuta katika soko la dunia pamoja na changamoto za usafirishaji wa mafuta kufuatia mvutano unaoendelea Mashariki ya Kati, hususan katika eneo la Mlango wa Hormuz.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa gharama za usafirishaji wa mafuta ziliongezeka kwa kiasi kikubwa mwezi Juni, hali iliyochochea kupanda kwa bei za dizeli licha ya kushuka kwa bei ya petroli katika soko la ndani.

Serikali imeendelea kutoa ruzuku ya Sh534.91 kwa kila lita ya dizeli ili kupunguza athari kwa sekta za uzalishaji, usafirishaji wa bidhaa na huduma za usafiri wa umma
football clubs

03/06/2026

Shout out to my newest followers! Excited to have you onboard! Ally Nassor, Hassani Mkongwa, Amiri Amiri

 : Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Moscow nchini Urusi kwa ajili ya zia...
03/06/2026

: Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewasili jijini Moscow nchini Urusi kwa ajili ya ziara ya kiserikali yenye lengo la kuhimarisha zaidi uhusiano wa muda mrefu wa kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na kihistoria ulipo kati ya nchi hizo mbili.

Mwanahabari wetu Benjamin Mzinga anatuarifu kuwa, Rais Samia atafanya mazungumzo rasmi na mwenyeji wake, rais Putin, katika Ikulu ya Kremlin jijini Moscow. Mazungumzo hayo yatajikita katika kuimarisha ushirikiano katika sekta za kimkakati, ikiwemo biashara na uwekezaji, elimu, sayansi na teknolojia, nishati, madini, kilimo, miundombinu na utalii.

football clubs

  Mwanafunzi wa kidato cha nne wilayani Chato mkoani Geita anadaiwa kubakwa baada ya kukamatwa na kuingizwa katika hifad...
02/06/2026

Mwanafunzi wa kidato cha nne wilayani Chato mkoani Geita anadaiwa kubakwa baada ya kukamatwa na kuingizwa katika hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato na Mwanaume aliyekuwa na nia ya kuitapeli fedha familia ya Binti huyo.

Tukio hilo limetokea wakati binti huyo wa kidato cha nne akirejea nyumbani kuchukua madaftari Kutoka katika Kijiji cha Imalabupina alikopangishiwa na wazazi wake kwani shule anayosoma ipo umbali wa kilometa zaidi ya tisa, na Kijiji hicho kimepakana na hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato.

Mtuhumiwa alikuwa na kitu chenye ncha kali kinachosadikika kuwa ni moko na alimteka nakumuingiza kwenye hifadhi hiyo kisha kumfanyia kitendo hicho cha ukatili.
football clubs

HT://CAF U17 AFRICA CUP OF NATIONS 2026Fainali  30’ Senegal 🇸🇳 0️⃣-1️⃣🇹🇿 Tanzania ⚽️Hamisi Chenga   football clubs
02/06/2026

HT://CAF U17 AFRICA CUP OF NATIONS 2026

Fainali

30’ Senegal 🇸🇳 0️⃣-1️⃣🇹🇿 Tanzania
⚽️Hamisi Chenga

football clubs

Match updates:Final Afcon-u17Senegal 0-1 Tanzania⚽️ Razaki Juma 4'  football clubs
02/06/2026

Match updates:Final Afcon-u17
Senegal 0-1 Tanzania
⚽️ Razaki Juma 4'
football clubs

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa...
02/06/2026

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiagana na viongozi mbalimbali katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam, kabla ya kuondoka nchini kuelekea Shirikisho la Urusi kwa ziara ya kitaifa itakayofanyika kuanzia tarehe 3 hadi 5 Juni 2026.

Ziara hiyo inafanyika kwa mwaliko wa Rais wa Shirikisho la Urusi, Mheshimiwa Vladimir Putin, na inalenga kuimarisha ushirikiano na mahusiano ya kidiplomasia kati ya Tanzania na Urusi.

football clubs

  Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ambazo zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii...
01/06/2026

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa imetoa ufafanuzi kuhusiana na taarifa ambazo zinasambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu Chama cha Mapinduzi (CCM) kuigomea Ofisi hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya Ofisi ya Msajili wa nchini kuiandikia barua rasmi Chama cha Mapinduzi (CCM), ikikitaka kutoa maelezo na ufafanuzi wa kina kufuatia kauli iliyotolewa na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, inayodaiwa kukiuka Sheria ya Vyama vya Siasa.

Kwa mujibu wa msajili msaidizi wa vyama vya siasa, Sisty Nyahoza, Ofisi ya Msajili ilikipa chama hicho ukomo wa hadi Mei 29 2026, kuandika maelezo yake rasmi ambapo tayari imewasilisha majibu ya barua hizo Mei 19, 2026 katika Ofisi ya Msajili.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty
Nyahoza, ametoa ufafanuzi huo leo Juni 1, 2026 na kudai taarifa hiyo ya CCM kuigomea Ofisi hiyo zipuuzwe
football clubs

HABARI:Aliyekuwa Diwani wa kata ya shelui Wilaya ya Iramba mkoan SINGIDA Bi . Agnes Amosi Amefariki Dunia Ghafla mei 30 ...
01/06/2026

HABARI:Aliyekuwa Diwani wa kata ya shelui Wilaya ya Iramba mkoan SINGIDA Bi . Agnes Amosi Amefariki Dunia Ghafla mei 30 .
Akiandika katika katika ukurasa wake wa instagram waziri mkuu wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Mwigulu Nchemba ameeleza "Nimepokea kwa Masikitiko makubwa taarifa za kifo cha diwani wa kata ya Shelui dada yetu Agnes Amos poleni wanafamilia na wanachi wa kata ya Shelui".
football clubs.

Address

Mwananyamala
Temeke

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Modern football clubs. posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category