Binam Sports Updates

Binam Sports Updates Contact information, map and directions, contact form, opening hours, services, ratings, photos, videos and announcements from Binam Sports Updates, Sports, Moshi, Shanti Town.

karibuni Sana hapa ndugu zangu katika page hi ya MICHEZO hapa utapata update zenye kuaminika ulimwenguni pote Tetesi za usajili nk matokeo ya MICHEZO Duniani kote utayapata hapa usitoke yajayo Yana furahisha Beka Maujuz jr Mtu maarufu

Mathias Pogba (32) ambaye ni kaka wa nyota wa Juventus Paul Pogba (29) anashikiliwa na Polisi kuhusiana kula njama akiwa...
15/09/2022

Mathias Pogba (32) ambaye ni kaka wa nyota wa Juventus Paul Pogba (29) anashikiliwa na Polisi kuhusiana kula njama akiwa na rafiki zake na kutaka kumuibia mdogo wake Paul

Kiungo huyo wa zamani wa Manchester United alidai mwezi uliopita kuwa alikuwa muathirika wa njama ya pauni milioni 11 iliyokuwa ikipangwa na marafiki zake wa utotoni pamoja na kaka yake.

Kwa mujibu wa gazeti la Le Monde Mathias alijisalimisha mwenyewe kwa Polisi wa Ufaransa wanaofanya uchunguzi wa kesi hiyo.

✍Chelsea inaandaa pendekezo la mkataba wa kocha Graham Potter kwani kipaumbele kikuu kitakuwa kujadili mradi wa muda mre...
07/09/2022

✍Chelsea inaandaa pendekezo la mkataba wa kocha Graham Potter kwani kipaumbele kikuu kitakuwa kujadili mradi wa muda mrefu🚨.

Graham Potter anachukuliwa k**a kipenzi kikuu cha Chelsea k**a kocha mpya atakayemrithi Tuchel .

Mauricio Pochettino sasa anasubiri Chelsea iamue hatima maana yeye kafunguka kuwa yuko tayari.

Brighton waliipa ruksa Chelsea kufanya mazungumzo na kocha Graham Potter na watajadiliana na Chelsea kuhusu fidia baada ya makubaliano na kocha huyo.

Source Fabrizio Romano.

Ameandika  Bingwa wa kubalansi.....imagine alichaguliwa kuwa mwamuzi bora last season. Kwanini hakumpa kadi ya pili ya n...
06/09/2022

Ameandika

Bingwa wa kubalansi.....imagine alichaguliwa kuwa mwamuzi bora last season. Kwanini hakumpa kadi ya pili ya njano Banyana kwa rafu mbaya dhidi ya Morrison? Hata rafu ya kwanza ya Banyana kwa Job ilistahili Red. Alipomaliza kuwaumiza Yanga Mungu akamuumbua. Dube akakatwa katika boksi na Bakari. Penalti ya wazi kabisa. Hakuwa na jinsi. Kuwaridhisha Yanga akakataa penalti ya Azam. Ya Morrison? Halali kwa sababu kulikuwa na contact from behind na mlinzi wa Azam hakugusa mpira. Siku nyingine ikitoka orodha ya waamuzi wanaokwenda Afcon halafu wa kwetu hawapo usiniulize maswali. Otherwise Kipre Junior ni mtu na robo. Feisal duh mashuti ya moto yashakuwa mazoea kwake.

Mtandao wa Foot+257 kutoka nchini Burundi umeripoti  kuwa Simba wapo katika mazungumzo Pitso Mosimane ili kuchukua na na...
06/09/2022

Mtandao wa Foot+257 kutoka nchini Burundi umeripoti kuwa Simba wapo katika mazungumzo Pitso Mosimane ili kuchukua na nafasi ya kocha Zoran Maki

Wakati klabu ya Simba ikiachana na aliyekuwa kocha wake Maki Zoran, inaelezwa kuwa beki wa klabu hiyo Mkenya Joash Onyan...
06/09/2022

Wakati klabu ya Simba ikiachana na aliyekuwa kocha wake Maki Zoran, inaelezwa kuwa beki wa klabu hiyo Mkenya Joash Onyango amegoma kufanya mazoezi na Klabu yake ya Simba SC akishinikiza kuvunja Mkataba na Klabu hiyo baada ya kuambiwa hayupo kwenye mipango na aliyekuwa kocha mkuu wa klabu hiyo,Zoran Maki.

Licha ya uongozi wa Klabu ya Simba SC 🇹🇿 kumtaka Beki huyo kujiunga na wenzake kambini Jumamosi ya wiki iliyopita lakini beki huyo amesimamia msimamo wake wa kutaka kuvunja Mkataba wake na huku taarifa zilizopo ni Kuwa Tayari ameshapeleka barua kwenye Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ili waweze kumsaidia suala lake.

➡️Taarifa za Simba kumtimua Zoran bila shaka zitakuwa zimepekewa kwa shangwe sana na Onyango, huenda akarudi kambini.

Klabu ya Simba Sc imefikia makubariano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na makocha wao wote watatu kocha wao mkuu ...
06/09/2022

Klabu ya Simba Sc imefikia makubariano ya pande zote mbili ya kuvunja mkataba na makocha wao wote watatu kocha wao mkuu zoran maki kocha wa viungo na kocha wa makipa.

🚨BREAKING Manchester United imethibitisha kukamilisha usajili wa winga wa Ajax Antony kwa ada ya €95m pamoja na nyongeza...
30/08/2022

🚨BREAKING

Manchester United imethibitisha kukamilisha usajili wa winga wa Ajax Antony kwa ada ya €95m pamoja na nyongeza ya €5m na mkataba hadi June 2027 wenye nafasi ya kuongeza mwaka mmoja hadi 2028.

🚨UPDATES  Chelsea na Barcelona wapo katika mazungumzo ili kufikia makubaliano ya ada ya uhamisho na mkataba wa Aubameyan...
30/08/2022

🚨UPDATES

Chelsea na Barcelona wapo katika mazungumzo ili kufikia makubaliano ya ada ya uhamisho na mkataba wa Aubameyang kwenda Chelsea, mazungumzo bado yanendelea,

Marcos Alonso ameaimbia Chelsea hakuna chaguo lingine zaidi yeye anataka tu kuhamia Barcelona.

Source Fabrizio Romano.

Kuna uwezekano mkubwa wa Antony kuwepo kwenye mechi ya Alhamisi kati ya Man Utd Na Leicester City kwani Visa na kibali c...
30/08/2022

Kuna uwezekano mkubwa wa Antony kuwepo kwenye mechi ya Alhamisi kati ya Man Utd Na Leicester City kwani Visa na kibali chake cha kufanyia kazi tayari kinashughulikiwa, taarifa itatolewa hivi karibuni 🚨.

Source Sky Sports.

Anaandika. ahmedally_ Juzi kati niliona tangazo la UTO la kutafuta Afisa Habari Mwenye Degree 👏👏Nilishangaa tangu lini U...
30/08/2022

Anaandika. ahmedally_

Juzi kati niliona tangazo la UTO la kutafuta Afisa Habari Mwenye Degree 👏👏

Nilishangaa tangu lini UTO wakaajiri msomi

Lakini nikafurahi kuona sasa UTO wanataka kuachana na Maafisa Habari WANAO BWABWAJA😤

Ni hatua kubwa kwao ambayo wameiga kwetu

Wamejifunza kwetu namna Afisa habari msomi anavyoweza kuendesha mpira wa kisasa

Tangu mwanzo naingia Simba, UTO walikua wanan’gan’gana huyo Ahmed ni wa kwetu, kaenda huko kutafuta riziki nikawajibu mnapenda kuwa na mtu k**a mimi

Hatimae na nyie mmetafuta shule ije isemee mpira na huo ndo muongozo wa Club Licensing

Haiwezekani unakua na Afisa Habari ambae akienda kwenye Press unashika roho mkononi na kujiuliza leo sijui atagombana na nani au atamtukana nani?

Unakua na Afisa Habari mmoja lakini Wanasheria 10 wanasubiri kumtetea akitukana watu

Sio kila anaeweza kuongea kwa sauti anaweza kuwa Afisa habari k**a mtu ana sauti kubwa anaweza kuwa hata kondakta lakini Afisa Habari atuachie tuliokaa darasani na tukafaulu

Hata mwenyezi Mungu anasema hawawezi kuwa sawa anaejua na asieujua!!!

Sasa mlete Degree kweli tutakagua Chuo alichosoma!!

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Guinea Matthias Pogba jumamosi usiku alienda katika mitandao ya kijamii na kutoa taarifa...
29/08/2022

Nyota wa zamani wa kimataifa wa Guinea Matthias Pogba jumamosi usiku alienda katika mitandao ya kijamii na kutoa taarifa kuhusu mdogo wake nyota wa timu ya Taifa ya France, Paul Pogba.

Matthias amesema Pogba alimtuma aende kwa mganga ili akamloge mshambuliaji wa timu ya Taifa ya France Kylian Mbape.

Tayari mamlaka husika zimeanza kufanya uchunguzi kuhusu sakata hilo.

Pogba nae amesema kaka yake Matthias alikuwa kwenye genge la majambazi ambalo limewahi kujaribu kutaka kumuibia dola za Marekani milioni 13, Paul amesema majambazi ambao kaka yake alikuwa nao ni marafiki zake wa utotoni kwa pamoja walijaribu kutaka kufanya unyang'anyi wa kiasi hicho cha pesa.

Taarifa kutoka Yanga zinadai, Lazarous Kambole 🇿🇲 amesajiliwa akiwa ni majeruhi wa muda mrefu bila mabosi wa Jangwani ku...
28/08/2022

Taarifa kutoka Yanga zinadai, Lazarous Kambole 🇿🇲 amesajiliwa akiwa ni majeruhi wa muda mrefu bila mabosi wa Jangwani kulijua hilo mapema. Kambole hayuko fiti na kuna tetesi za Mabosi wa Yanga SC kushusha Mshambuliaji mwingine mpya.

Address

Moshi
Shanti Town

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Binam Sports Updates posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category