25/03/2026
Sehemu ya 1: "SIRI YA CHUMBA NAMBA 302"
GPA VS PENZI LA SIRI
"NILIDHANI NIMEPAKIWA KWENYE BODABODA KWENDA 'HOSTEL' KUPUMZIKA BAADA YA MTUHAN WA UE, KUMBE NDIO NAANZA SAFARI YA KUIPOTEZA NDOA YA DEAN WETU WA WANAFUNZI..."
(The Story - Sehemu ya Kwanza):
Ilikuwa ni Jumanne ya saa 11 jioni, jua la Chuo Kikuu likiwa limeanza kuzama. Nilikuwa nimechoka vibaya baada ya pambano la saa tatu la mtihani wa Cost Accounting. Nilichokuwa nawaza ni kufika hostel, nile "Wali-Maharage" wangu, kisha nilale mpaka asubuhi.
Nikiwa nimesimama getini namsubiri bodaboda wangu wa kila siku, gari aina ya Range Rover nyeusi ilipaki mbele yangu. Kioo kikashuka taratibu. Alikuwa ni Dr. Malisa, Dean wetu wa Wanafunziβmwanaume ambaye chuo kizima kinamheshimu kwa msimamo na ukali wake.
"Sophy, unapokwenda ni mbali na giza linaingia. Ingia nikutupe hostel," alisema kwa sauti yake ya mamlaka lakini safari hii ilikuwa na kaukaribu fulani.
Sikuwa na hiyana, nikaingia. Lakini tulipoingia barabara kuu, Dr. Malisa hakukata kona ya kuelekea hostel. Alinyoosha kuelekea upande wa mjini.
"Doctor, mbona tunapita huku?" nilimuuliza kwa sauti ya kutetemeka.
Alitabasamu kidogo, tabasamu ambalo sijawahi kuliona darasani. "Kuna mzigo wangu nataka niuchukue kule 'Apartments' za jirani, nisaidie kuubeba kisha nitakurudisha. Usijali."
Tulipofika kwenye jengo lile la kifahari, chumba namba 302, Dr. Malisa alifungua mlango na kuniambia niingie. Nilichokikuta ndani hakikuwa "mzigo" wa vitabu wala mafaili.
Kwenye kochi la sebuleni, alikuwa amekaa Sarah, rafiki yangu kipenzi (Roommate wangu) ambaye aliniambia anaumwa yuko hostel amelala. Alikuwa amevaa "Night dress" nyepesi, na kwenye meza kulikuwa na chupa ya Wine na glasi mbili.
Sarah alistuka kuniona, akasimama haraka. Lakini kabla hajasema lolote, Dr. Malisa alifunga mlango kwa 'lock' ya ndani, kisha akavua koti lake na kusema...
"Sophy, karibu kwenye familia. Sasa hivi siri ya Sarah ipo mikononi mwako, na siri yako inaanza sasa hivi..."
Moyo ulinitoka. Nilijua hapa si salama, lakini mlango ulikuwa umeshafungwa.
ITAENDELEA SEHEMU YA 2...Je, unahisi Dr. Malisa ana mpango gani na Sophy? Na kwa nini Sarah (Roommate) yuko pale?
K**a unataka nishushe SEHEMU YA 2 saa hivi, dondosha comment ya "NEXT" hapa chini! #