Sports extra large

Sports extra large Sports bar πŸ’ͺπŸ’ͺ😎

Ubaya ubwela
25/06/2025

Ubaya ubwela

08/03/2025
Kuna Nyakati tofauti tofauti iliyopita kwenye Ardhi ya soka Tanzania Uwezo na vipaji vya washambuliaji mbali mbali wamep...
07/03/2025

Kuna Nyakati tofauti tofauti iliyopita kwenye Ardhi ya soka Tanzania Uwezo na vipaji vya washambuliaji mbali mbali wamepita ligi kuu Tanzania bara na baadhi bado wapo Mfano John Bocco, Fiston Mayele, Meddy Kagere yupi kwako alikuwa Mshambuliaji wako pendwa..?

Hilo ndio kikosi cha wachezaji wanao pewa sifa azistahili mpaka sasa ligikuuu katika tim tatu simba yanga azam 1. Mohamm...
07/03/2025

Hilo ndio kikosi cha wachezaji wanao pewa sifa azistahili mpaka sasa ligikuuu katika tim tatu simba yanga azam

1. Mohammed mustard
2.kelvin kijiri
3chadrack boka
4.abdul razak Hamza
5.yoro
6.fabrice ngoma
7.kibu
8.Jean charles
9.ateba
10 nassor saadun
11.prince dube

Naona awa watu wapewa sifa zisizo stahili mfano kibu na chasambi mukwala na ateba dube na mzize yani akuna usawa Ndo ivo kila mtu ana nyota yake

Nyota wa Yanga wanatakiwa kuongeza umakini wakati wakipambania ushindi, Jumamosi katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya...
15/01/2025

Nyota wa Yanga wanatakiwa kuongeza umakini wakati wakipambania ushindi, Jumamosi katika mchezo wao wa mwisho wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya MC Alger kutokana na rekodi ya ajabu ya mwamuzi, Patrice Milazare kutoka Mauritius πŸ‡²πŸ‡Ί ambaye anatarajiwa kuamua mchezo huo.
Katika michezo mitatu aliyoamua msimu huu, rekodi ya Milazare ni ya kutisha, hakuna timu yoyote iliyofunga bao, hivyo kocha wa Yanga, Sead Ramovic na vijana wake wanatakiwa kufanya kazi ya ziada kuhakikisha wanabadilisha rekodi hiyo kwani uhitaji wao wa kushinda ni mkubwa kulinganisha na wapinzani wao MC Alger hata sare inawabeba.
Katika michezo aliyochezesha msimu huu, Milazare aliongoza mechi mbili muhimu za kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, Oktoba 10, 2024, Ghana walikuwa wenyeji wa Sudan matokeo yalikuwa 0-0.. Mwezi mmoja baadaye, Milazare alichezesha mechi nyingine kati ya Libya na Benin matokeo 0-0.
Mchezo wa tatu wa msimu huu kwa Milazare ulikuwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika, na MC Alger walicheza ugenini dhidi ya TP Mazembe huko DR Congo. Katika mechi hiyo, hakuna timu iliyofunga bao na mechi hiyo ilimalizika 0-0.
Kulingana na rekodi za mwamuzi huyo, kila hatua itahitaji umakini wa ziada ili kupambana na si tu wapinzani wao MC Alger, bali pia na mwamuzi huyu ambaye ni k**a vile β€˜mfalme wa suluhu

Kwenye viwango vya timu bora barani Afrika chini ya CAF, Yanga wana alama 34 mpaka sasa na ikitokea Yanga wamefuzu kwend...
14/01/2025

Kwenye viwango vya timu bora barani Afrika chini ya CAF, Yanga wana alama 34 mpaka sasa na ikitokea Yanga wamefuzu kwenda robo fainali watafikisha alama 39 na kuzishusha timu 2 kwenye top 10 ya CAF. Na ikitokea Yanga wamefika nusu basi wataingia 5 bora ya CAF. Misimu 3 ya KIBABE.

Kimahesabu Ya Yanga ni kushinda mechi mbili zilizobaki ila Kuna Ugumu mkubwa Sana nauona,,,,na Huenda yakajirudia Yale y...
06/01/2025

Kimahesabu Ya Yanga ni kushinda mechi mbili zilizobaki ila Kuna Ugumu mkubwa Sana nauona,,,,na Huenda yakajirudia Yale ya CR BELOUZIDAD,,,,Maana Yangu ni Hii,,,,,,
MC Algeria ana Point 5 endapo atashinda Mechi ijayo na Mazembe atakuwa na Point 8,,,,,,,,,,,
Yanga Akicheza na Al Hilal ikitokea Yanga kapata Sare Atakuwa na Point 5,,,,,
Mechi ya Mwisho itakuwa Benjamin Mkapa,,,,ambapo Yanga ataingia Uwanjan akiwa na Point 5 hivyo atatakiwa Kumfunga MC Algeria Goli 3_0 atakuwa ikitokea Hivyo Yanga Kafuzu ila Kikubwa ni Mechi ya Al hilal tusipoteze Tupate Point la Sio Tatu Bas Moja Alaf mechi ya mwisho,,,,,,Iwe Afe kipa Afe Beki MC Algeria Afungwe Chuma 3-0

Wengi mnasema Al Hilal anafungika kwake ila sio Rahisi k**a wengi mnavyofikiria,,,,,Jamaa Wapo vzr sana nadhan mpka hapo Kuna watu wamenielewa k**a Sio point Tatu bas tupate Moja πŸ™Œ

Huenda yakajirudia Yale Yale ya CR BELOUZIDAD,,,,,kwamba Head to Head itaamua

πŸ–ŠοΈSpSports extra large

𝗕π—₯π—˜π—”π—žπ—œπ—‘π—š π—‘π—˜π—ͺ𝗦: π—–π—Ÿπ—˜π— π—˜π—‘π—§ π— π—­π—œπ—­π—˜ π—žπ—¨π—©π—”π— π—œπ—ͺ𝗔 𝗑𝗔 π— π—”π—¦π—›π—”π—•π—œπ—žπ—œ π—ͺ𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗦𝗖Mashabiki na Wanachama wa Yanga waishio Jijini Dar ea Sala...
04/01/2025

𝗕π—₯π—˜π—”π—žπ—œπ—‘π—š π—‘π—˜π—ͺ𝗦: π—–π—Ÿπ—˜π— π—˜π—‘π—§ π— π—­π—œπ—­π—˜ π—žπ—¨π—©π—”π— π—œπ—ͺ𝗔 𝗑𝗔 π— π—”π—¦π—›π—”π—•π—œπ—žπ—œ π—ͺ𝗔 π—¬π—”π—‘π—šπ—” 𝗦𝗖

Mashabiki na Wanachama wa Yanga waishio Jijini Dar ea Salaam, wamekubaliana kuwa siku ya kesho wanaenda kuvamia Duka la Mchezaji wao Clement Mzize lililopo Sinza ili Kununua Mzigo wote uliopo Dukani na kuacha Duka likiwa Tupu.

Shida nyingine imewasili hapa mjini,timu nyingi zimenza kunyanyasika zikikutana na Yanga.Chini ya makocha wawili waliopi...
29/12/2024

Shida nyingine imewasili hapa mjini,timu nyingi zimenza kunyanyasika zikikutana na Yanga.

Chini ya makocha wawili waliopita (Nabi & Gamond) Yanga walicheza mpira wa pasi nyingi,Yanga walikuwa na utaratibu wa kuwatongoza wapinzani kwa pasi nyingi kabla ya kufunga magoli (TIP TAP FOOTBALL) ila chini ya Ramovic tunashuhudia pira β€œGegen-Pressing” au kwa kizungu tunasema β€œCounter-pressing).

-Yanga ya Ramovic haitaki pasi 10 kufika kwenye lango la mpinzani,badala yake inahitaji pasi tatu hadi nne kufika kwako na kukufunga✍️

-Yanga ya Ramovic haitaki back-pass wala Sideway pass,mchezaji akiiba mpira ni kwenda mbele Yanga wako direct sana✍️

-Yanga ya Ramovic haipigi cross nyingi za juu,badala yake mashambulizi mengi yanatokea pembeni kwa fullbacks na wingers kisha zinapigwa V-pass kwenye 12 na viungo washambuliaji wanafunga…..rejea magoli mawili ya Pacome leo✍️

JINSI GANI YANGA WANAWEKA MTEGO KABLA YA KUFANYA PRESSING?

Mara nyingi tumezoea kuona mstari wa kwanza wa namba 9 na 10 ukianzisha pressing kwa walinzi wa timu pinzani,ila Yanga ya Ramovic,inasubiri wapinzani wafike kati kati ya uwanja kisha viungo wazuiaji (Aucho na Muda) wanaweka pressure kwa mchezaji mwenye mpira huku walinzi wa kati (Job na Bacca) wakisogea kati kati ya uwanja kukata passing option…..baada ya kuiba mpira unapigwa pembeni kwa mawinga na fullbacks kisha shambulizi linaanzia hapo✍️

Ndugu zangu huu mpira wa Yanga una magoli mengi ya β€œTurnovers” wapinzani wanafanyishwa makosa mengi na kuhadhibiwa.

Nimeanza kuelewa kwanini Yanga waliwakomalia Widad Casablanca.Ukweli ni kwamba Mzize ni mchezaji mwenye thamani kubwa kw...
25/12/2024

Nimeanza kuelewa kwanini Yanga waliwakomalia Widad Casablanca.

Ukweli ni kwamba Mzize ni mchezaji mwenye thamani kubwa kwenye safu ya ushambuliaji ya Yanga.

Mzize anacheza K**a right-winger,Left-winger na number 9.

Mzize anakupa kasi,mashuti,pressing,magoli na nguvu ya kukimbia k**a kichaa uwanjani…..siyo kila mchezaji ana mapafu k**a Mzize.

Leo kaweka goli la 5 la NBC Premier League.

Ni basi Watanzania tumeamua kuwasifia akina Dube,Ateba na Mukwala Ila Mzize ni mshambuliaji bora mzawa kwa sasa.

Msimu huu ametulia sana mbele ya goli….na tukumbuke huyu bado ni kijana Wa miaka 20

Anaandika Mchambuzi wa Michezo kutoka Crown FM, Hans Rafael.✍️

🚨⚠️Haitochukua muda Wananchi wataanza tena kurejea ule mpira wao na mabao yao, haitochukua muda kabla Clement Mzize aanz...
25/12/2024

🚨⚠️Haitochukua muda Wananchi wataanza tena kurejea ule mpira wao na mabao yao, haitochukua muda kabla Clement Mzize aanze kupokea ofa nyingi huko nje, haitochukua muda kuanza kutenganisha maji na mafuta, haichukui muda kugundua Prince Dube kamba zote hajafunga penati, haitochukua muda timu zitaanza kuitwa Matawi.

K**a hii hali itaendelea haitochukua muda jina la GSM na udhamini kuanza kuwa kiitikio kwenye ule wimbo maarufu, haitochukua muda kusikia Marefa na TFF wote ni Wananchi, haitochukua muda sanaπŸ˜€

Address

Mwanza

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Sports extra large posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share