FREDY MSUHA

FREDY MSUHA WORK HARD IN SILENCE AND LET THE SUCCESS MAKE NOISE

15/04/2025

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro limetoa ufafanuzi wa picha mjongeo (video clip) iliyoonekana kusambaa kwenye mitandao ya kijamii ikihusisha watu waliokuwa wanatumia gari lenye namba za usajili T.540 EHF aina ya Toyota Noah ikidaiwa walikuwa wakijaribu kumteka kijana mmoja aitwaye Jonathan Ayo (37), mkazi wa KCMC Moshi eneo la Mbuyuni Wilaya ya Moshi Manispaa Aprili 12, 2025.

Taarifa ya leo Aprili 14, 2025 iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoani humo imeeleza kuwa baada ya kupokea taarifa hiyo Jeshi hilo lilifanya ufuatiliaji mara moja na kufanikiwa kuwak**ata watu wawili ambao ni Kelvin Temu (39), mkazi wa KCMC Moshi na Samson Magere (30), mkazi wa Soweto Moshi wakiwa na gari T.540 EHF aina ya Toyota Noah inayodaiwa kuhusika katika tukio hilo ambapo Gari hilo linamilikiwa na Kampuni ya KESSA TOURS yenye ofisi zake mtaa wa Soweto Moshi Mjini.

Uchunguzi wa tukio hilo umebaini kwamba tukio hilo halikuwa la utekaji bali Watuhumiwa hao walikuwa wamemuajiri Jonathan Ayo anayedaiwa kutekwa k**a mtaalam wa mifumo (I.T) wa kampuni yao ambapo tarehe 06 Aprili, 2025 alikwenda ofisini kwao mtaa wa Soweto kuchukua kompyuta mpakato (Laptop) ya ofisi akieleza kuwa anataka kufanyia kazi za ofisi akiwa nyumbani kwake na angeirudisha kesho yake.

Baada ya Ayo kuondoka na laptop hiyo hakuirudisha ndipo waajiri wake walipata mashaka na walianza kumtafuta kwa siku tano bila mafanikio. Ilipofika tarehe Aprili 12, 2025 walifanikiwa kumpata akiwa Bar mtaa wa Rau akinywa pombe ambapo alikubali kwenda kuwakabidhi laptop hiyo na alifanya hivyo.

Watu hao wakitumia gari T.540 EHF aina ya Noah baada ya kuipata laptop yao waliamua wampeleke Polisi ndugu Ayo kwa hatua zaidi na walipofika eneo la Mbuyuni majira ya saa moja usiku Ayo alifungua mlango wa gari ikiwa imesimama kwenye foleni na kujaribu kukimbia akiwa anapiga kelele za wezi zilizopelekea Wananchi kuwashambulia watu hao ambapo Askari Mgambo aliyekuwa eneo hilo alifanikiwa kuzuia vurugu hizo na kumfikisha Ayo kituo cha Polisi Moshi.

Karibuni kujiandikisha kuwa mpigakura.
11/10/2024

Karibuni kujiandikisha kuwa mpigakura.

19/06/2024

Mwigizaji maarufu wa Nigeria Yul Edochie(42) ambaye ameoa wake wawili, ameibuka kusema ndoa sio kitu cha lazima kwa kila mtu na wala sio sahihi mtu kuvumilia yasiyotakiwa kuvumiliwa hadi kufia ndani ya ndoa

Yul ambaye ni mtoto wa mkongwe wa filamu Pete Edochie anasema k**a ndoa yako ina amani ni sawa ila ukiona ndoa imekuwa chungu kwako achana nayo, baadaye ukikutana na mtu mwingine ukaona anafaa ingia nae kwenye ndoa na ukiona pia baadaye mambo hayaendi vizuri ndani ya ndoa ya pili toka ingia tena kwenye ndoa hata mara 50 kikubwa ni furaha yako

Anasema huwezi kudhibiti maneno ya watu wataongea nini juu yako na pia katika maisha kinachompa furaha mtu sio kinachompa furaha mtu mwingine hivyo angalia wewe na maisha yako sio wakupangie uishije wakati ndoa imekuwa mwiba kwako

Kwa mwingine mke wa kwanza wa Yul anadai talaka yake na wameelezwa kutengana baada ya kuletewa mke wa pili ingawa Yul ameshasema hakuoa mke wa pili ili kuchukua nafasi ya mke wa kwanza

07/06/2024
11/05/2024

Rais Yoweri Museveni wa Uganda, ameiagiza Wizara ya Ukaguzi wa Serikali na Maadili, kuchunguza utajiri wa Spika wa Bunge la nchi hiyo Anita Among ambao inasemekana ameficha nchini Uingereza.

Serikali ya Uingereza iliwapiga marufuku kusafiri nchini Uingereza Spika huyo na Mawaziri wawili wa zamani Mary Goretti Kitutu na Agnes Nandutu na mali zao kuk**atwa kwa kile ilichokiita kielelezo cha ufisadi na hakina nafasi katika jamii.

Gazeti la Nile Post lilifichua Jumanne Mei 7, kwamba Benki kuu ya UAE pia ilikuwa imetoa onyo kwa taasisi zote za kifedha kuzuia shughuli zozote zinazofanywa na Mawaziri hao wawili Nandutu na Kitutu.

Katika barua ya Mei 2 kwa Waziri wa Mambo ya Nje Jeje Odongo, Bw Museveni amesema alikuwa na mkutano wa dharura na Kamishna Mkuu wa Uingereza, Bi Kate Airey OBE, katika Ikulu ya Nakasero siku ambayo Serikali ya Uingereza ilitangaza vikwazo hivyo.

Mbarikiwe, mwenyezi Mungu awaongoze katika njia sahihi.
11/05/2024

Mbarikiwe, mwenyezi Mungu awaongoze katika njia sahihi.

08/05/2024

WORK HARD IN SILENCE AND LET THE SUCCESS MAKE NOISE.

08/05/2024

KAWAIDA KABISA 💪

🔋𝐌𝐖𝐀𝐌𝐁𝐀 Joseph Guede mchezaji bora 𝐍𝐈𝐂 𝐈𝐍𝐒𝐔𝐑𝐀𝐍𝐂𝐄 𝐏𝐋𝐀𝐘𝐄𝐑 𝐎𝐅 𝐓𝐇𝐄 𝐌𝐎𝐍𝐓𝐇 kwa Mwezi wa Aprili


Address

Mbinga

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when FREDY MSUHA posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Share

Category