07/04/2026
Hongera wanamichezo wote kwa juhudi kubwa mlizoonyesha uwanjani! πͺβ½
Mchezo kati ya Magunga 0 dhidi ya Milani 1 umehitimishwa, na licha ya matokeo, bado mmeonesha moyo wa kupambana, nidhamu na uzalendo wa hali ya juu. Kumbukeni, ushindi sio mwisho wa safari bali ni hatua, na kushindwa sio mwisho bali ni funzo la kujijenga zaidi.
Kwa timu ya Magunga, pigeni moyo kondeβkila changamoto ni nafasi ya kujirekebisha na kurudi imara zaidi. Kwa Milani, hongereni kwa ushindi, endeleeni kudumisha kiwango na nidhamu.
Twendeni tukazidi kushirikiana, kujifunza na kuendeleza vipaji vyetu kwa ajili ya maendeleo ya mpira wetu wa wilaya. π₯β½
Mpira unaendelea, safari bado ndefu!