06/06/2026
๐จKOCHA wa Simba, Steve Barker, amefanya mabadiliko ya muundo wa kikosi chake yanayomuhusu sana Elie Mpanzu ambaye Jumapili iliyopita ya Mei 24, 2026 aliwapa Wekundu hao wa Msimbazi ushindi, akisema sasa Mkongomani huyo atakuwa anacheza k**a mshambuliaji wa kati.
Mechi tatu zilizopita za Simba, Barker amemuondoa Mpanzu kutoka kucheza k**a kiungo anayeshambulia akitokea pembeni na sasa anamuanzisha eneo la mshambuliaji wa kati, mabadiliko ambayo yamemrudisha benchi mshambuliajia halisi Seleman Mwalimu.
Akizungumzia mabadiliko hayo, Barker ameliambia Mwanaspoti kuwa, kwasasa Mpanzu ni mmoja wa washambuliaji wake wa kati ambapo atakuwa anamtumia eneo hilo kuiongezea timu hiyo ubora.
Barker amesema anataka safu yake ya ushambuliaji iwe na watu wenye kasi ambao mara wanapounasa mpira wanatakiwa kukimbia haraka kwenda kushambulia wakati ambao wapinzani wanakuwa bado hawajajipanga sawasawa.
โMpanzu ni mmoja wa washambuliaji wetu kwasasa, nakubaliana na wewe kwamba alikuwa anatumika kuna wakati akitokea pembeni lakini sasa atakuwa anacheza hapo, kuna kitu bora zaidi tunakilenga kutoka kwake,โ
โTunahitaji watu wenye kasi zaidi kule mbele ambao wakati timu pinzani ikipoteza mpira, tunatakiwa kuwa na kasi ya haraka kwenda kuwashambulia kabla hawajajipanga sawasawa na hili limekuwa linafanyika sawasawa.โ