29/08/2022
: Wak**atwa na polisi kwa madai ya kutaka kumpindua Mwenyekiti wa shirikisho la Soka kambini
Baadhi ya viongozi kwenye k**ati ya Wenyeviti wa vilabu wamek**atwa Jumatatu hii Agosti 29, 2022 kwa tuhuma za kupanga njama za kutaka kumpindua Mwenyekiti wa shirikisho la soka, Bwana Abbé MAYELE KINOIS; kambini hapa mkoani Kigoma.
Taarifa kutoka kwa baadhi ya watu wa karibu na viongozi wa jamii wahusikao na michezo zimethibitisha hilo kwa kusema kuwa k**ata k**ata hiyo imefanyika mida ya saa saba mchana ambapo zaidi ya watu wawili ndio wamepelekwa kituo cha polisi A ili kwenda kujibu shtaka linalowakabili la kufanya kikao cha kupanga mapinduzi ya kumuondoa Bwana Kinois bila kupata kibali toka Ofisi ya Mkuu wa kambi.
Afisa mmoja wa polisi ambaye hakupenda kutaja jina lake amesema; "Hawa viongozi wenu wanacheza na serikali. Tuliwasambaza hiyo jana pale kwenye ukumbi wa vijana walipokutana bila barua ya ruhusa toka serikalini. Nimesikia eti ni zaidi ya vikao viwili wamefanya bila kuwa na kibali."
Kuk**atwa kwa viongozi hao wa k**ati ya Wenyeviti wa vilabu kunakuja wakati huu ambapo zaidi ya asilimia 95 ya Wenyeviti wa vilabu vyote vya daraja la kwanza na la pili kambini hapa wamekuwa wakimpinga bwana Kinois kutokana na uongozi wake mbaya ambapo Wenyeviti hao wa vilabu waliwayi kukutana Agosti 9, 2022 kwenye kikao cha kuamua kuomba Mwenyekiti wa shirikisho pesa walizochangiza kwa ajili ya washindi wa ligi ya Nyarugusu Cup daraja la kwanza na la pili ili washindi hao wapate haki yao na kuhamua kumkataa bwana Abbé MAYELE KINOIS.
Vigogo hao waliwayi kuandikia bodi ya michezo barua wakionyesha kuwa Kinois hafai kuwa Kiongozi wa shirikisho kambini kutokana na makosa mengi anayoyafanya ikiwemo kula rushwa pande zote na kujikopa hela ya kuendesha ligi bila kuzirejesha. Majibu ya barua hiyo ya Wenyeviti wa vilabu yalionekana kuchelewa ndipo wakaamua kuandaa kikao hicho ambacho kimepelekea baadhi ya waandaaji wacho ambao majina hayajajulikana kuonja maabusu.