07/12/2024
MC ALGER VS YANGA.
~ Kipindi cha kwanza wanetu wa Yanga wamechezewa nusu uwanja aloo yanga waliwaacha sana MC Alger acheze mpira ni kitu ambacho hakikua kizuri kwenye game plan ya mwalimu Ramovic.
~ kipindi cha kwanza Pacome Zouazoua amepewa kadi ya njano ya kujitakia kabisa kwenye ile dakika ya 23'
~ Dakika 30 za mwanzo Yanga waliwaacha MC Alger wacheze wanavyotaka afu wao kazi yao ilikua kuzuia , baada ya dakika 30 za mwanzo Yanga wakafunguka na wao kuanza kucheza mpira
~ MC Alger walikua fasta sana kurudisha mali baada ya kupoteza mali ni wepesi sana kukaba na kurudisha mpira tena kwenye imaya yao.
~ Kuna mwamba anaitwa Delort anavaa jezi namba 9 ni alikua moto sana good game kwake, Kwa Yanga ibra bacca alooo ni moto sana kwenye lile eneo la ulinzi pale Yanga.
HT MC ALGER 0 : 0 YANGA
~ Nimependa ile fair play ya mtu mmoja kutoka benchi la ufundi kwa Yanga alikua akiongea na ball boys pape hii ndiyo maana halisi ya mchezo wa mpira wa miguu.
~ Kipindi cha pili kilivyo anza MC Algers walianza kwa moto sana, kuna mwamba anavaa jezi namba 11 alooo alikua moto sana ile winger machachali mno huyo Tayeb Meziani.
~ Poor marking kwa Yanga inawapa goli Mc Alger kulitia captain wao Ayoub Abdelloui mnamo dakika ya 64' piga goli flani hivi la kichwa baada ya mpira wa freekick.
~ Mabeki wa Yanga kuna muda walikua wamechoka walai mpaka Djigui alikua na kazi nyingine tena ya kufanya afanye marking yeye mwenyewe.
~ Wanetu ball boys walianza kuzingua kuanzka dakika ya 70' ya mchezo , na waarabu wakaanza kulala pale uwanjani kwenye izo dakika baada ya kupata bao lao la kuongoza .
~ Yanga hili tatizo la namba 9 asilia bado linawatesa sana pale mbele , nimeona mipira inayofika hakuna wamaliziaji pale mbele.
~ Dakika ya 78' aliingia Sofuine Bayazid na Kipre Junior sasa pale game plan ya mwalimu wa MC Alger ilikua kutumia mawinga ila apate matokeo kwenye dakika 10' za mwishoni, ila lengo lao halikufanikiwa yanga wakakaza
~ Poor marking ile ile Kipre Junior chupu chupu awaweke kamba pale, yanga mashambulizi tena.Chama chupu chupu awaweke kamba sio bahati kwao yanga.
~ Dakika za jioni Djigui Diara amepewa kadi ya Njano ni ya kujitakia kabisa angekausha , Chama pia amepewa kadi ya njano sahihi kabisa alifanya madhambi.
~ MC Algers wakapata bao la pili kupitia Sofuine Bayazid jezi namba 7 goli la kikatili kabisa na kumaliza mchezo.
~ Yanga haijaisha mpaka iishe sisi waTanzania tupo pamoja na nyinyi Yanga mpaka mwisho wa safari hii ya ligi ya mabingwa Africa 🌍, Yanga poleni kwa kupoteza mchezo wa pili kwenye hatua za makundi ya CAF CHAMPIONS LEAGUE bado kuna mechi 4 mbele tunaimani mtafanya vizuri zaidi na ziaid.
~ Yanga mpaka sasa hivi anadaiwa magoli manne atatoboa kweli?
FULL TIME MC ALGER 2 : 0 YANGA