19/11/2025
*_ELIMU YA KUTAFUTA (INDIRECT EDUCATION)_*
Hii ni Elimu ambayo huipata kiumbe kwa kujifunza kutoka katika vyanzo mbalimbali k**a vitabu, shule, N.k na Elimu hii tumejaaliwa zaidi sisi wanadamu kuliko viumbe wengine.
e.g ili umiliki gari lazima ujifunze namna ya kuliendesha, ili ujue kutibia magonjwa lazima usome udaktari, ili uwe na mahusiano bora na mpenzi wako lazima usome elimu ya Ndoa N.k
sasa Aina hii ya elimu imegawanyika katika makundi au Njia kuu tatu.
๐ *AL-MA'ARIFATU SHUHUDIA* (ANA KWA ANA)
Hapa mtu hupata elimu kwa kujifunza ana kwa ana kupitia matendo yote yenye kuhusisha mifumo yote ya fahamu (macho, masikio, pua, mdomo, Ngozi nk, ikiwa ni kusoma vitabu, majarida, kusikiliza hadithi au mwalimu mashuleni. e.g huwezi kujua harufu fulani bila kunusa kwa pua, huwezi kujua ladha ya kitu fulani isipokuwa umeionja, vilevile huwezi kusoma na kuandika isipokuwa umejifunza kwanza.. wala kujua dhambi ni nini isipokuwa umesoma au kufundishwa na mtu.
๐ *AL-FAWDIA*(AKILI)
Hii ni elimu anayopata Mtu kwanjia ya kiakili tu. mfano ni pale mtu anapochezea sarafu chooni bila kujua madhara yake kisha ianguke shimoni alafu utambuzi ukamjia kwamba hatakiwi kuchezea sarafu sio tu chooni bali maeneo yote hatarishi.. Hapo anakuwa amepata utambuzi kwa kufikirsa akili binafs bila kufundishwa wala kusoma katika kitabu.
Na mara nyingi hutokea pale mtu anapokumbwa na changamoto ndogo ndogo na kubwa kubwa kiujumla.