17/04/2026
Timu nane za hatua ya robo fainali CRDB Bank Federation Cup zishapatikana, leo Ijumaa Aprili 17 inafanyika droo ili kujua nani na nani watakutana.
Droo hii itafanyika kuanzia saa 6:00 mchana na kuruka mbashara kupitia AzamSports1HD.
Timu zilizofuzu hatua ya robo ni Yanga SC, Simba SC, Azam FC, Singida United, TRA United, JKT Tanzania, Mashujaa FC, na Coastal Union.