02/09/2026
Mvutano wa Marekani na Iran: Makombora Yanaruka, Lakini Usafirishaji wa Mafuta Haujasimama.
Mapigano kati ya Marekani na Iran yalisababisha bei ya mafuta kupanda mfululizo kwa wiki mbili, lakini wiki hii kasi hiyo imegonga mwamba...
Bei ya mafuta ghafi aina ya Brent ilipanda kutoka katikati ya dola 80 hadi karibu dola 97, huku Marekani na Iran zikiendelea kushambuliana karibu na Mlango-Bahari wa Hormuz.
Kisha jambo moja muhimu sana likatokea: meli ziliendelea na safari zake.
Afisa mmoja wa Marekani alisema takriban meli 40 zilipita kwenye mlango-bahari huo jana zikiwa zimebeba mamilioni ya mapipa ya mafuta, hata wakati makombora na ndege zisizo na rubani (drones) zikirushwa huku na kule.
Marekani ilishambulia takriban maeneo 100 ndani ya Iran, ikiwemo meli mbili za mafuta za serikali chini ya sera mpya ya Rais Trump ya meli kwa meli (tanker for tanker policy), ambapo drones zilishambulia vyumba vya injini vya meli hizo.
Iran ilijibu mapigo kwa kurusha takriban makombora ya masafa marefu (ballistic missiles) 25 na drones zilizolenga kambi za Marekani, lakini mengi yalitunguliwa au kudondoka bila kusababisha maafa.
Wafanyabiashara walipoona kwamba mafuta bado yanasafirishwa, taharuki ilipungua. Bei ya mafuta ya Brent ilishuka kutoka karibu dola 97 hadi chini ya dola 95.
Hata hivyo, hakuna anayechukulia hali hii k**a shwari. Bei ya gesi barani Ulaya imefikia kiwango cha juu zaidi katika kipindi cha miaka 3, na tayari Ulaya inahofia janga jingine la kupanda kwa gharama za maisha.
Mafuta bado yanaendelea kusafirishwa, na kwa sasa, jambo hili linaonekana kudhibiti hofu ya soko isiwe kubwa zaidi.
Follow Swahili Prime Ent