27/04/2026
Mchezaji wa kulipwa wa mchezo wa Softball, ndugu akikabidhi jezi ya team yake Spikes ya nchini Czechia ama Czech Republic kwa Katibu wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) katika ofisi za Baraza hilo mapema leo hii. Mchezaji huyo alipita kutoa salamu na shukrani zake kutokana na juhudi zinazofanywa na serikali katika kukuza michezo na vipaji mbalimbali kupitia Baraza hilo.
Ndugu anakuwa Mtanzania wa kwanza katika historia kucheza mchezo huo katika bara la Ulaya, ikumbukwe kwamba kabla ya kuelekea nchini Czechia, alikuwa akiitumikia inayoshiriki ligi kuu ya mchezo wa baseball hapa Tanzania.
Tukiwa k**a Chama, kwa niaba ya uongozi, wadau na wachezaji wote tunaungana kwa pamoja kumpa hongera mtanzania huyu anaekipiga huko majuu.