13/12/2025
🕊️ Taarifa ya Masikitiko | Soka la Afrika Limeguswa
Klabu ya Yanga na familia ya soka kwa ujumla imepata pigo kubwa baada ya kupokea taarifa za kifo cha aliyekuwa nyota wao wa zamani, Chico Ushindi, aliyefariki leo akiwa nyumbani kwao Lubumbashi – DR Congo 🇨🇩.
Chico atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alipokuwa akiitumikia TP Mazembe, baadaye Yanga SC, na hivi karibuni akiwa mchezaji wa FC Bazano ya Ligi Kuu ya Congo.
Kifo chake ni pengo kubwa katika soka la Afrika.
Pumzika kwa amani, shujaa wa soka. 🤍⚽