21/04/2026
Imefichuliwa: Jürgen Klopp, Mauricio Pochettino na Didier Deschamps ndio makocha wanaoongoza kupewa nafasi k**a Real Madrid wataamua kutompa nafasi ya kuendelea Álvaro Arbeloa, kwa mujibu wa .
“Meneja wa timu ya taifa ya Marekani, Mauricio Pochettino, bado ni chaguo kubwa, anaheshimika sana na Florentino Pérez, na mkataba wake unaendelea hadi baada ya Kombe la Dunia la majira ya joto,” ripoti hiyo inaeleza.
“Jürgen Klopp pia anawavutia viongozi wa Madrid, ingawa yeye na wakala wake wamekuwa wakikanusha taarifa hizo mara kwa mara, wakisema ameridhika na nafasi yake ya sasa katika Red Bull.”
“Didier Deschamps pia ametajwa k**a mgombea. Kocha huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa amekuwa madarakani tangu 2012, na mkataba wake unaisha baada ya Kombe la Dunia.”