Namkoveka10

Namkoveka10 Professional swimming Coach for learn to swim and competition incl people with disabilities. I am trying to be best I can be and deliver best services

Kozi ya Viongozi kutoka kwa Kamati ya kimataifa ya Paralympic (IPC) imeanza rasmi jijini Dar es Salaam hii siku ya Ijmaa...
11/09/2026

Kozi ya Viongozi kutoka kwa Kamati ya kimataifa ya Paralympic (IPC) imeanza rasmi jijini Dar es Salaam hii siku ya Ijmaa tarehe 11.09.2026 katika Colosseum Hotel, hapa Dar es Salaam

Viongozi wa k**ati ya Paralympic (TPC) wanakutana pamoja ili kuimarisha uongozi na kujenga msingi imara zaidi wa kukua kwa Michezo ya Watu Wenye Ulemavu (Para Sport) kote nchini Tanzania.

Ikiwezeshwa na Mkufunzi wa IPC Bw. Holger Losch kutoka Afrika Kusini.

Viongozi Imara Zaidi. Miundo Imara Zaidi. Michezo ya Watu Wenye Ulemavu Imara Zaidi.

InclusiveSport Leadership ParaSport

Hakuna fahari kubwa k**a kupata nafasi ya kuweka nguvu, akili na uzoefu wako kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yako. S...
02/09/2026

Hakuna fahari kubwa k**a kupata nafasi ya kuweka nguvu, akili na uzoefu wako kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi yako. Safari njema kwangu na kwa ustawi wa Taifa letu.

Karibu Ndani ya Familia ya TPC, Dr. Janeth Mlay! Mstari wa mbele kuelekea mafanikio mapya unazidi kuimarika! Kamati ya P...
30/06/2026

Karibu Ndani ya Familia ya TPC, Dr. Janeth Mlay!

Mstari wa mbele kuelekea mafanikio mapya unazidi kuimarika! Kamati ya Paralympic Tanzania (TPC) tunafarijika na kufurahia sana kukukaribisha Dr. Janeth Mlay katika familia hii kubwa ya Para-Sports ukiwa ni Mkurugenzi wa ufundi na mjumbe wa k**ati ya utendaji ya TPC..

Tunaamini kwa pamoja tutaandika historia mpya ya mafanikio, kuibua vipaji, na kuweka viwango vya juu vya kiutendaji na kiufundi katika michezo ya watu wenye ulemavu nchini.

Kazi ndio kwanza inaanza! Let’s make history together! 🚀🔥

PamojaTunaweza

21/06/2026

Just kumbukizi ya miaka 20 ya Dar Jogging Club

Chama cha Sitting Volleyball kinaendesha mafunzo maalum katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Hii ni fursa ya kipe...
21/06/2026

Chama cha Sitting Volleyball kinaendesha mafunzo maalum katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM). Hii ni fursa ya kipekee kwa wote wenye nia na shauku ya kuendeleza mchezo wa Paravolley nchini!

Michezo ya watu wenye ulemavu inahitaji nguvu yetu sasa hivi. Ni wakati wetu wa kuamka, kuwajibika, na kuonyesha uwezo wetu.

Tarehe: 24 - 28 Mahali: Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)

Usikae pembeni! Jiunge nasi sasa tufanye mapinduzi kwenye Paravolley. Karibuni wote! 🙌🔥

InclusivityInSports

UONGOZI MPYA: KARIBU KATIBU MKUU! 🔔Tunapenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Ndugu Ramadhan Namkoveka kwa kuchag...
18/06/2026

UONGOZI MPYA: KARIBU KATIBU MKUU! 🔔

Tunapenda kuchukua fursa hii kumpongeza kwa dhati Ndugu Ramadhan Namkoveka kwa kuchaguliwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa Kamati ya Utendaji ya Tanzania Paralympic Committee (TPC).

Udumu katika kuiongoza michezo ya walemavu na kuifikisha katika kilele cha mafanikio nchini na kimataifa. Kila la heri katika majukumu haya mapya ya kujenga na kuendeleza vipaji!

11/06/2026

Nyota wetu wa kuogelea baharini (Open Water Swimming), Lo**ta, ametoa mtazamo wake kuhusu Mashindano ya hivi karibuni ya Africa Aquatics Open Water Swimming Championship yaliyofanyika nchini Mauritius.

Lo**ta amepongeza waandaaji kwa maandalizi ya hali ya juu na kuonyesha jinsi mashindano hayo yalivyokuwa na ushindani chanya na wenye kiwango kikubwa.

Hata hivyo, k**a mchezaji aliyekuwepo uwanjani (maji makuu), Lo**ta hakusita kuangazia changamoto mbalimbali walizokutana nazo waogeleaji wakati wa mashindano hayo. Changamoto hizi ni darasa tosha na chachu ya kujifunza na kujiandaa vyema zaidi kwa mashindano yajayo ya kikanda na kimataifa!

AthletePerspective

11/06/2026

Mwamuzi wa Kimataifa (ITO), Coach Ramadhani Namkoveka, ameeleza utayari wa kuleta mapinduzi ya kiufundi nchini baada ya kukamilisha usimamizi wa mashindano ya pamoja ya African Aquatics na Zone 4 Open Water Championship nchini Mauritius.

Licha ya kuishukuru Tanzania kwa fursa hiyo, Coach Ramadhani amesisitiza kuwa maendeleo ya kweli yanahitaji usimamizi madhubuti:

"Ukweli ni kwamba kanuni za World Aquatics lazima zifuatwe na kutumika kwa 100% ." Yale yote aliyojifunza na kuyatumia kimataifa, anajipanga kuyasogeza kwa wadau wa nyumbani kupitia:
Makocha: Kuboresha mbinu za maandalizi ya wanariadha.
Waamuzi: Kusimamia sheria kwa viwango vya juu vya kimataifa.
Waogeleaji: Kuelewa kanuni na mazingira halisi ya mashindano makubwa.

Maarifa haya yanakwenda kuwa chachu kubwa ya maendeleo ya Open Water nchini Tanzania!

TechnicalOfficial

10/06/2026

Baada ya mapambano makali kwenye mawimbi ya Mauritius, Kocha wa Timu ya Taifa ya Open Water, Khalid Rushaka, ametoa tathmini yake mapema leo kabla ya timu kupaa kurejea Tanzania.

Kocha ameonyesha kuridhishwa na hatua kubwa iliyopigwa na waogeleaji wetu, hasa katika upande wa kuboresha muda wao wa mashindano.

Lakini kazi haishishii hapa! Ili kufika mbali zaidi, Kocha Rushaka amesisitiza mpango wa kuweka nguvu ya pamoja na makocha wa vilabu ili kukuza zaidi viwango vya wachezaji, kuongeza idadi ya waogeleaji wa open water ili kuvuna medalil mbeleni.

Safari ya mafanikio ndio kwanza inaanza! Karibuni nyumbani mashujaa wetu

07/06/2026

LO**TA BOREGA ANAENDELEA KUANDIKA HISTORIA! 🇹🇿

Kwa mara ya pili mfululizo, nyota wetu wa kuogelea kwenye bahari (Open Water Swimming), Lo**ta Borega, amezitikisa anga za kimataifa kwenye mashindano ya African Aquatics Open Water Swimming Championship! 🏊‍♀️💨

Kwenye mchujo mkali wa mita 3000 (3km Sprinting), Lo**ta amepambana kiume na kuingia kwenye Top 20 bora ya Africa waliokata tiketi ya NUSU FAINALI! Huku akionyesha upinzani mkali dhidi ya miamba kutoka Egypt, South Africa, Namibia, na wenyeji Mauritius.

Huyu si binti wa mchezo mchezo—anazidi kuitangaza na kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kishujaa! Euro, mawimbi na upepo wa baharini havijamzuia kuweka rekodi zake.

Hongera sana Lo**ta, timu nzima ya ufundi pamoja na makocha, na TSA! Watanzania tupo nyuma yako kuelekea nusu fainali! 🇹🇿🔥

**taBorega KuogeleaTanzania FlyTheFlag

Address


Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Namkoveka10 posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

  • Want your business to be the top-listed Gym/sports Facility?

Share