27/02/2026
Mkurugenzi wa makampuni ya Jayrut, Joel Wegasira, ameibua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kupost picha akiwa sambamba na basi jipya aina ya Irizar, huku akionesha hati ya kusafirisha gari hiyo kwa njia ya meli kuja Bandari ya Dar es Salaam. ๐ข๐ฅ
Kupitia ukurasa wake, Joel aliandika kwa kujiamini:
โLas acciones hablan mรกs que las palabras ๐โ
yaani, โMatendo yanaongea zaidi ya maneno ๐โ
Kisha akaongeza ujumbe mzito:
โCanโt wait to deliver the Best to My Best Team โ โค๏ธ๐ฆ
Kauli hiyo imechochea shauku kubwa kwa mashabiki wa Simba Sports Club, maarufu k**a Mnyama. Wengi wanaamini hili ndilo basi jipya la kisasa litakaloibeba timu yao kwenye safari za mashindano ya ndani na kimataifa.
Mitandao ya kijamii imefurika pongezi na maswali โ je, hili ndilo basi kali kuliko yote kuwahi kumilikiwa na klabu hapa nchini? Je, litawasili lini rasmi Dar es Salaam?
Kilicho wazi ni kwamba presha imepanda, na mashabiki wa Simba wanasubiri kwa hamu kuona โmzigoโ huo ukitia nanga bandarini.
Wangapi wana hamu ya kuliona basi jipya la Mnyama? ๐ฆ๐ฅ
Follow mpira wetu