Free Will Tv

Call Website Contact the business

Free Will Tv Karibu kwa habari za Michezo

🚨Kiungo wa zamani wa Manchester City na timu ya taifa ya Uhispania, David Silva ametangaza rasmi kurejea uwanjani na kut...
08/10/2026

🚨Kiungo wa zamani wa Manchester City na timu ya taifa ya Uhispania, David Silva ametangaza rasmi kurejea uwanjani na kutengua uamuzi wake wa kustaafu soka uliodumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

➡️Silva mwenye umri wa miaka 40, amelazimika kurejea daluga zake akisaini mkataba wa muda mfupi wa kujiunga na klabu ya Supreme Sha Tin inayoshiriki Ligi Kuu ya Hong Kong.

➡️Mnamo Julai 2023 Silva alitangaza kustaafu soka akiwa na klabu ya Real Sociedad kutokana jeraha kubwa la goti alilolipata wakati wa maandalizi ya msimu mpya.

🚨Klabu ya Simba haitambui mfumo wa tiketi ulioanza kuuza tiketi za mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati yao dhidi ya Yanga SC...
08/10/2026

🚨Klabu ya Simba haitambui mfumo wa tiketi ulioanza kuuza tiketi za mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati yao dhidi ya Yanga SC, Oktoba 10, 2026.

➡️Bodi ya Ligi TPLB wamerejea kwa mzabuni (Vendor) wa awali licha ya kusema mfumo wake haujafanya kazi kwa ufanisi.

➡️Bodi ya Ligi TPLB imeanza tena kutumia mzabuni wa awali wa mfumo wa tiketi ambaye katika kikao cha awali wao kulichofanyika jana wenyewe walieleza kuwa hakuwa amefanya kazi kwa ufanisi uliotarajiwa na ndiyo maana walitangaza tenda na kupata mzabuni mpya mwingine.

➡️Cha kushangaza hatua hii inakuja baada ya Simba SC kuwasilisha barua rasmi kwa Bodi ya Ligi TPLB, ikieleza kwa kina malalamiko na mapungufu iliyoona kwenye mfumo huo.

➡️Hadi sasa Simba SC haijapata majibu rasmi ya barua hiyo kutoka kwa Bodi ya Ligi TPLB na kwenye kikao cha maandalizi ya mchezo huo CEO wa Bodi ya Ligi aliulizwa maswali na hakutoa majibu.

➡️Maswali ya Kujiuliza, Kwanini mzabuni ambaye awali alielezwa kuwa hakufanya kazi vizuri anarejeshwa?, Ni nini kimebadilika tangu kikao hicho?, Kwanini malalamiko rasmi ya Simba SC hayajajibiwa kabla ya mfumo huo kuanza kutumika tena?

➡️Simba SC wanasema hili ni suala linalogusa moja kwa moja maslahi ya mashabiki, mapato ya serikali, klabu na uendeshaji wa mfumo wa tiketi hivyo kunahitajika uwazi.

07/10/2026

Ahmed Ally ni zaidi ya cheka Tu....

🚨Afisa Habari wa klabu ya  Simba SC, Ahmed Ally amesema kwa sasa anachoweza kuwaahidi mashabiki wa klabu hiyo ni ushindi...
07/10/2026

🚨Afisa Habari wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally amesema kwa sasa anachoweza kuwaahidi mashabiki wa klabu hiyo ni ushindi katika mechi ya Dabi ya Kariakoo itakayopigwa Oktoba 10, 2026.

➡️Ahmed amesema anaamini ushindi huo utatokana na ubora wa kikosi cha Simba walichonacho kwa sasa, huku akisisitiza kuwa timu ipo tayari kwa mchezo huo.

- Haya ni maneno ya Ahmed Ally Afisa habari wa klabu ya Simba..

07/10/2026

Kuelekea Dabi Salma Ndo Mtangazaji .....

Weka maoni yako hapa chini....

Credit

07/10/2026

Kikosi cha Twiga Stars kimeonda asubuhi ya leo kuelekea Botswana tayari kwa Mchezo wa kufuzu michuano ya Olimpiki los Angeles mwaka 2028.

🚨Nyota wa timu ya taifa ya  Ureno Cristiano Ronaldo ameeleza kwa undani kilichotokea kati yake na kocha wa Portugal, aki...
07/10/2026

🚨Nyota wa timu ya taifa ya Ureno Cristiano Ronaldo ameeleza kwa undani kilichotokea kati yake na kocha wa Portugal, akisema kwamba kuvunjwa kwa ahadi ndiyo hatimaye kulikokuwa sababu ya yeye kuamua kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa.

➡️Ronaldo anakiri kwamba alifanya kosa kwa kutowasalimia mashabiki baada ya mchezo na anaomba msamaha kwa watu wa Portugal na wachezaji wenzake.

"Naomba msamaha kwa wachezaji wenzangu kwa kuondoka. Jukumu ni langu peke yangu, FPF inapaswa kuniadhibu bila sababu zozote za kupunguza adhabu; kwa kuwa mimi ni nahodha, hilo ni jambo linaloongeza uzito wa kosa"

🎙️“Nitakuwa tayari, k**a ambavyo nimekuwa tayari siku zote, baada ya kumaliza adhabu yangu, , nitakuwa tayari kushindana na kushinda kwa ajili ya timu yetu ya taifa.”

➡️Hata hivyo, anasisitiza kwamba hajawahi kuingilia maamuzi ya kocha na anasema kwamba, ikiwa atakuwa fiti na anacheza baada ya kumaliza adhabu yake, atajitokeza tena kwa ajili ya timu ya taifa ya Portugal.

🚨Afisa wa Habari wa  klabu ya  Simba SC, Ahmed Ally, amevunja ukimya na kukanusha uvumi unaosambaa ukidai kuwa mshambuli...
07/10/2026

🚨Afisa wa Habari wa klabu ya Simba SC, Ahmed Ally, amevunja ukimya na kukanusha uvumi unaosambaa ukidai kuwa mshambuliaji wao Libasse Gueye amepata majeraha kuelekea Dabi ya Kariakoo. Ahmed Ally amewatoa hofu mashabiki wa Wekundu wa Msimbazi kwa kusisitiza kuwa nyota huyo yuko salama wa salmin, hajaumia hata ukucha na yuko kwenye utayari wa hali ya juu kwa ajili ya mapambano ya mwezi huu wa Oktoba baada ya kikosi kurejea salama kutoka kambini nchini Afrika Kusini.

➡️​Akitangaza maandalizi ya mchezo huo wa watani wa jadi utakaopigwa Oktoba 10, Ahmed Ally amethibitisha kuwa pambano hilo litatimua vumbi katika Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam kuanzia saa moja kamili usiku. Kwa sasa kikosi kimejichimbia kambini Mbweni na kinaendelea na programu kali za mazoezi katika Uwanja wa Mo Simba Arena, huku akiwasihi mashabiki kujipatia tiketi zao mapema kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa TFF ili kuepuka usumbufu.

➡️​Hata hivyo, msemaji huyo amebainisha kuwa mchezo huu wa dabi ndicho kipimo halisi cha kiwango cha timu yao msimu huu na Simba inahitaji ushindi kwa kila hali ili kujiweka vizuri kwenye mbio za ubingwa.

🚨Taarifa zinealeza kuwa Klabu ya Yanga imemfungulia mashtaka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mchezaji wake anay...
07/10/2026

🚨Taarifa zinealeza kuwa Klabu ya Yanga imemfungulia mashtaka katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) mchezaji wake anayocheza nafasi ya beki wa kulia, Israel Mwenda, kwa tuhuma za utoro kazini.

➡️Kwa mujibu wa chanzo, Yanga SC inadai kuwa imefanya jitihada mbalimbali za kumtafuta mchezaji huyo, lakini hadi sasa haijui alipo, huku akiwa bado ana mkataba na klabu hiyo.

➡️Kutokana na hali hiyo, Yanga SC imeamua kulifikisha suala hilo TFF ili hatua zaidi zichukuliwe kwa mujibu wa taratibu.

Address


Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Free Will Tv posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Free Will Tv:

Shortcuts

  • Want your business to be the top-listed gym/sports facility?

Share