01/09/2026
Mwezi wa nane umeisha na mjadala umeenea kwenye soka: kati ya Libasse Gueye na Maxi Nzengeli, kwamba nani anastahili kutwaa tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi.
Wote wameonyesha kiwango kizuri katika mechi zao tano, lakini kila mmoja ana takwimu zinazompa sababu ya kuamini kuwa tuzo hiyo inamstahili.
Twende kwenye hesabu. 👇
🔴 LIBASSE GUEYE — MFALME WA ASSISTS
Katika michezo 5, Libasse Gueye amefunga goli 1 na kutoa assists 5.
Hiyo inampa jumla ya goal contributions 6 ndani ya mechi tano.
Kwa wastani, ni 1.2 goal contribution kwa kila mechi.
Lakini kuna jambo moja linaloweza kumzuia kus-win mjadala huu:
katika mechi hizo tano, Libasse amefanikiwa kuchukua tu tuzo 2 za Man of the Match.
Hii inaonyesha kwamba licha ya kuwa na mchango mkubwa katika kutengeneza magoli, si kila mchezo alikuwa yeye ndiye aliyebeba spotlight.
Kwa kifupi:
1 GOLI ⚽ + 5 ASSISTS 🅰️ = 6 GOAL CONTRIBUTIONS
Takwimu za creation? 🔥
Mchango kwenye magoli? 🔥🔥
Libasse ana kesi yake.
________________________________________
🟢 MAXI NZENGELI — MASHINE YA MAN OF THE MATCH
Kwa upande mwingine, Maxi Nzengeli amekuwa na mwezi ambao unaweza kumfanya kila shabiki aanze kuuliza swali moja:
"K**a si yeye, ni nani?"
Katika michezo 5, Maxi amefunga goli 3, akiwa hana assist.
Lakini hapa takwimu nyingine zinaingia na kubadilisha kabisa mjadala:
Maxi amekusanya tuzo 5 za Man of the Match katika mechi 5.
Ndiyo.
Mechi 5 → Man of the Match 5. 🤯
Hiyo inaashiria kiwango cha juu cha ushawishi binafsi katika kila mchezo kwa mujibu wa takwimu hizi.
Kwa upande wa mchango wa mabao:
MAGOLI 3⚽⚽⚽ + 0 ASSISTS = 3 GOAL CONTRIBUTIONS
Kwa hiyo, kwenye goal contributions, Libasse anamzidi.
Lakini kwenye Man of the Match, Maxi anaongoza kwa tofauti kubwa.
________________________________________
⚖️ SASA, TUZO TUMPE NANI?
Ukiangalia goal contributions pekee, Libasse Gueye ana hoja nzito zaidi.
Mechi 5.Goli 1, Assists 5.
Goal contributions 6.
Lakini ukiangalia ushawishi wa mchezaji kwenye mechi moja moja, Maxi Nzengeli wa moto.
Mechi 5. Mabao 3. Na Man of the Match 5/5.
Kwa hiyo tunakuwa na picha mbili tofauti:
Libasse Gueye = Creator 🎯
Maxi Nzengeli = Match Winner 💥
Swali la msingi:
Je, Mchezaji Bora wa Mwezi anapaswa kuwa yule mwenye takwimu nyingi zaidi za kutengeneza magoli, au yule anayeonekana kuwa mchezaji bora zaidi katika mechi nyingi?
🏆 MAONI YETU JAMII SCORE
Kwa kuzingatia takwimu tulizotoa, Maxi Nzengeli ndiye anayestahili zaidi tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwezi wa Nane.
Si kwa sababu Libasse yupo chini—la hasha.
Libasse ana goal contributions nyingi zaidi, lakini Maxi ana hoja kizito sana kwenye mbanga hii
Kwa mtazamo huu, sisi tunampa:
🥇 MAXI NZENGELI — 55%
🥈 LIBASSE GUEYE — 45%
MAXI APEWE TU japo tofauti ni ndogo sana.
Au wewe unasemaje mdau ????. 👀