11/05/2023
Nchi umekubali kwa kauli moja ubora wa Bacca, Wachambuzi 99% wamesema ndio Man of the match.
"Mchezaji bora siku ya leo alikuwa Bacca, kwa sababu kabla ya mchezo wa leo hatari ya Marumo Gallants ilikuwa ni kwa striker wao, Ranga Chivaviro ambaye kwenye ligi ya Afrika kusini ameshafunga magoli (10) ..."
"... Akiwa miongoni mwa Wachezaji wa juu kabisa wanaoongoza kwa kufunga, kwa upande wa CAFCC ana maholi (5) sawa na Mayele, hivyo mpaka hapo ni mchezaji hatari"
"Kwa hiyo huyu mchezaji hatari alitakiwa awekewe ulinzi ili asiwe hatari, na hilo jukumu leo alipewa Ibrahim Bacca. Bacca leo amewania mipira mara (6) na akashinda (5) akipoteza mpira (1), na kwenye mipira hiyo amewania na Chivaviro mara (3) akashinda"
"Na katika mipira ya vichwa ameruka mara (6) huku ikipata (3) na katika yote hiyo ameruka na Chivaviro na akashinda.. Kwangu Bacca (25) ndiye Man of the match"
©️ Abissay stephen
Mchambuzi Kipenga extra EA-Radio
"Ibrahim Bacca leo sio tu alikuwa beki bora kwa Yanga Africa, ni mchezaji bora kwenye mechi.. Pamoja na sifa nyingi ambazo nimezitaja kuhusu Bacca, leo nimegundua pia kuwa ana leadership Quality"
"Kitambaa anacho Bakari Nondo, lakini Bacca anaongoza kwa matendo yake. Just wooow 🙌"
"Bacca ananifirisi maneno ana vitu vingi ambavyo vinamaanisha mchezaji wa kiwango cha juu. Anafanya vitu vingi kwa usahihi tena kwa muendelezo"
"Anazungumza sana, ana organize sana wenzake. Kwenye Mchezo huu Yanga wamefanya Tackles (15) na zimefanikiwa kwa (83%), Bacca amefanya clean Tackles (6). Anashinda vita zake angani na ardhini na ni mshindani kwelikweli"
©️ Wilson Oruma
Mchambuzi wa Efm radio
"Wananchi anytime wanaweza kutinga fainali aisee.. Game tough ya marudiano lakini mbili nyingi"
"Hawa Gallants ni watu na nusu, Yanga wawe makini lakini wana advantage kubwa .. Achana na bao la Aziz Ki na utundu wa kichaa msomi bwana Morrison katika bao la pili, lakini yule BACCA ni TOP TOP TOP defender"
©️ Edo Kumwembe
Mchambuzi wa Wasafi fm Radio