18/08/2026
Abiria waliotakiwa kusafiri kuelekea mkoani Kilimanjaro (Moshi) na Arusha kuanzia saa 3:00 na waliopaswa kuondoka na bus la saa 4:30 usiku kwa kutumia mabasi ya BM Coach, wajikuta kwenye wakati mgumu baada ya kuishia kusubiri hadi saa 8:00 usiku bila usafiri.
Akizungumza na KAU TV, abiria aliyejitambulisha kwa jina la Elida Mushi ameeleza jinsi ucheleweshaji huo ulivyowaingizia hasara kubwa, ikiwemo wengine kukosa fursa ya kushiriki mazishi na wengine kuchelewa kwenye maeneo yao ya kazi.
Unadhani makampuni ya usafirishaji yanapaswa kuchukuliwa hatua gani pindi kadhia k**a hii inapotokea?