23/04/2026
Cheti cha kuzaliwa ni hati rasmi inayothibitisha kuzaliwa kwa mtu, na ni muhimu sana kwa sababu kadhaa hapa Tanzania:
1. Kitambulisho Rasmi: Ni hati inayotambulika kisheria inayoonyesha tarehe na mahali pa kuzaliwa, pamoja na jina na taarifa za wazazi. Hii inasaidia kuthibitisha uraia wa mtu.
2. Elimu: Ni sharti la msingi kwa ajili ya kujiandikisha shule na kufanya mitihani ya kitaifa k**a vile darasa la saba, kidato cha nne, na kidato cha sita.
3. Huduma za Afya: Cheti cha kuzaliwa kinaweza kutumika kupata huduma za afya, hasa kwa watoto na wajawazito.
4. Ajira na Mafunzo:Waajiri wengi na vyuo vya ufundi na elimu ya juu huhitaji cheti cha kuzaliwa k**a sehemu ya mchakato wa maombi.
5. Usajili wa Ndoa:Linahitajika kwa ajili ya kuandikisha ndoa kisheria.
6. Hati za Kusafiria na Visa: Cheti cha kuzaliwa ni muhimu katika kupata hati ya kusafiria na visa kwa safari za kimataifa.
7. Mirathi: Husaidia katika masuala ya mirathi na haki za urithi, kwa kuwa kinaweza kutumika kuthibitisha uhusiano wa kifamilia.
Kwa kifupi, cheti cha kuzaliwa ni muhimu kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali na kuhakikisha haki za kisheria na kijamii zinapatikana kwa urahisi.
Unakipataje?
Unaweza kukipata sasa kwa kukiomba mtandaoni na baada ya muda mfupi ukakifuata ofisi za RITA zilizoko karibu na wewe.
Nini mahitaji muhimu?
Katika tangazo la picha tafuta viambata vitatu kati ya vilivyoanishwa huku barua ya utambulisho ikiwa na passport size kutoka kwa mtendaji wako wa kata ulipo ikiwa ni ya LAZIMA kati ya viambatanisho vinavyohitajika.
Nini gharama zake?
Itakugharimu tsh 30,000/= tsh 20,000 utalipa kwa Rita kupitia malipo ya serikali kwa njia ya control number utakayopewa, na tsh 15,000/= gharama za atakayekufanyia hiyo kazi na stationery.
Ni muda gani uli ukakikfuate ofisi za RITA baada ya kufanya maombi?
K**a taarifa zako ni kamili na hazina kikwazo inaweza kukuchukua siku 3 mpaka tano.
Wasiliana nami kwa namba 0687495993 au 0717963100 zote zipo whatsapp na unaweza kunipata muda wowote.
Link ya whatsapp inakuleta moja kwa moja
https://wa.link/ta3jwu