Cavion Nassir

Call Contact the business

Cavion Nassir 🎙️Sports Broadcaster & 📺 Digital Journalist |
| Correspondent 📝 🗞️

📝Bro to Bro (jinsia zote), nakuombea ushinde vita zote ambazo humwambii mtu yeyote kuwa unazipigana. And Remember, Hakun...
16/10/2026

📝Bro to Bro (jinsia zote), nakuombea ushinde vita zote ambazo humwambii mtu yeyote kuwa unazipigana. And Remember, Hakuna kinachodumu milele, Utashinda.

K**a nilivyoripoti hivi karibuni alipotoa Ahadi, Tajiri na Mwekezaji wa Simba SC, Mohammed Dewji leo amekamilisha malipo...
15/10/2026

K**a nilivyoripoti hivi karibuni alipotoa Ahadi, Tajiri na Mwekezaji wa Simba SC, Mohammed Dewji leo amekamilisha malipo ya bonasi ya Tsh. 500 Milioni aliyoahidi iwapo wangeshinda Dabi ya Kariakoo.

Hesabu za Kibindoni (Mechi 4 pekee):
🆚 Mighty Wanderers & Azam FC ➔ Milioni 700+


🆚 Yanga SC (Ushindi wa 2-1) ➔ Milioni 500


💵 Jumla Kuu: Tsh. BILIONI 1.2 za bonasi pekee!

Wachezaji na benchi la ufundi la Msimbazi mwezi huu wanaishi kwa bonasi tu, mishahara ipo intact!

NB: Simba ni Kula Maisha tu!

15/10/2026

⚽ “Mechi 11, Hakuna Bao!” — Je, Doumbia Anahitaji Muda Zaidi?

Ingawa ni kweli anahitaji muda kurejesha fomu yake, aina ya uchezaji wa Doumbia ndiyo inayoleta mashaka makubwa juu ya uwezo wake wa kufunga. K**a mtu aliyekuwa akimtetea kwa muda mrefu, haya ndiyo maoni yangu niliyoyatoa jana.

Nini mtazamo wako juu ya kiwango cha Doumbia kwa sasa?

Kuna mtu ana Mashaka na Ubora wa Yanga SC?Ni ngumu kwa timu kuwa imara kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa msimu, lazma kuna ...
15/10/2026

Kuna mtu ana Mashaka na Ubora wa Yanga SC?

Ni ngumu kwa timu kuwa imara kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa msimu, lazma kuna nyakati ambapo timu itayumba kidogo.

Inaweza kuwa bahati mbaya au nzuri kwa Yanga SC kujikuta kwenye nyakati hizi ngumu mwanzoni kabisa mwa msimu, jambo ambalo linampa kocha Mangqoba Mngqithi, benchi la ufundi, na wachezaji nafasi ya kujua nini cha kufanya ili kurejea kwenye ubora wao.

Ukiangalia kikosi mmoja mmoja na urejeo wa Stephane Aziz Ki, ubora mkubwa upo. Kwenye mchezo wa CAF Champions League dhidi ya CFFA siku ya Jumamosi, Yanga wana nafasi ya kurejesha utulivu mkubwa kwa kucheza soka safi na kupata idadi kubwa ya mabao. (Haitakuwa Rahisi, ubora wao utafanya kuwa nyepesi).

Mechi nne zilizopita dhidi ya Gaborone (michezo miwili), Geita Gold, na Simba SC zimeonesha mapungufu yao, na Jumamosi ndiyo sehemu sahihi ya kurekebisha makosa na kuanza upya kwenye msimu huu unaoendelea.

NB: Aziz Ki anarejea, Timu inaflow sana eneo la mbele akiwepo!

💣📝Katika kipindi hiki ambacho Duke Abuya yupo nje akijiuguza jeraha lake, huku Fred Duval Ngoma akiingia taratibu kwenye...
15/10/2026

💣📝Katika kipindi hiki ambacho Duke Abuya yupo nje akijiuguza jeraha lake, huku Fred Duval Ngoma akiingia taratibu kwenye timu (Bado) na Mudathir Yahya pamoja na Maxi Nzengeli wakibeba mzigo mkubwa eneo la kiungo,

Young Africans SC wanapaswa kumalizana mapema na Abubakar Salum ‘Sure Boy’ kwa kumlipa madai yake, kumalizana nae na kuweka tofauti hizo nyuma yao.

Kuumia kwa Abuya kunadhihirisha wazi kuwa Sure Boy bado ana mchango mkubwa. Licha ya uwepo wa Andambwile ambaye naye anahitaji muda wa kucheza (game time), Sure Boy ni mzoefu na ana uelewano wa hali ya juu (chemistry) na viungo waliopo k**a Maxi na Mudathir.

Wanahitaji suluhu katika eneo hilo na huenda likapatukana ndani ya Sureboy.

14/10/2026

Nilipomuuliza Kocha Steve Barker sababu ya Simba SC kurejea uwanjani baada ya mapumziko wakiwa na kasi kubwa na ufanisi wa hali ya juu, alibainisha kuwa siri haipo kwenye maelekezo ya vyumbani (halftime talk) pekee.

Kocha Barker ameeleza kuwa hayo ni matokeo ya jinsi wanavyocheza vizuri katika dakika 45 za kwanza wakiwachosha wapinzani wao, kuwapunguzia nguvu, na hatimaye kuwamaliza kipindi cha pili pale wanaposhindwa kuendana na kasi yao.

14/10/2026

⚽ “Mabao 17 kwenye mechi 5!”

Kocha Steve Barker anasema siri ya mafanikio yao ya kufumania nyavu Uwanja wa Uhuru ni ubora wa uwanja huo, uliowezesha timu yake kucheza soka la kasi waliyoipanga.

Barker anaamini katika viwanja vingine isingekuwa rahisi kufunga magoli mengi hivyo, lakini pia anasema walitambua namna ambavyo Mashujaa watakavyo approach mechi ya jana kwa kuzuia kwa idadi kubwa nyuma.

NB: Kuhusu Doumbia nina la kusema!

13/10/2026

Leo sina hata uchambuzi, Simba SC wamekuwa wakali sana msimu huu, Mechi 5 zilizopita wamefunga mabao 17, wameruhusu 3 pekee….

NB: Simba SC ukiwatazama kwenye TV hawatishi sana k**a ikiwaona live🔥 wamekuwa wamoto sana!

Kipindi cha kwanza bora sana kutoka kwa Simba SC! Walihitaji uvumilivu bila kutoka kwenye mpango wao pasi fupi fupi ziki...
13/10/2026

Kipindi cha kwanza bora sana kutoka kwa Simba SC! Walihitaji uvumilivu bila kutoka kwenye mpango wao pasi fupi fupi zikitafuta mianya kwenye ukuta wa Mashujaa FC. 🧠⚽

Katika mechi ngumu k**a hii, unahitaji ‘Individual Brilliance’; Libasse Gueye akawafungulia njia kabla ya Elie Mpanzu kupiga la pili na kuiweka Simba SC kwenye usukani kamili (Total Control).

Kwa upande mwingine, kadi nyekundu ya Hassan Kabunda imewatumbukiza Mashujaa FC na Kocha Aman Josiah kwenye dhahama nzito kuelekea kipindi cha pili! 🟥

Wakati mechi inapokuwa ngumu kuanzia filimbi ya kwanza kwa sababu ya uzuiaji imara wa mpinzani na uchovu kutoka kwenye m...
13/10/2026

Wakati mechi inapokuwa ngumu kuanzia filimbi ya kwanza kwa sababu ya uzuiaji imara wa mpinzani na uchovu kutoka kwenye mechi zilizopita (Derby) unahitaji wakati wa “Boom Shakalaka” kutoka kwa wachezaji wako tegemeo ili kuvunja kufuli la Magoli.

Libasse Gueye anafanya yake! Anacheka na nyavu kwa bao lake la 2 msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara (sasa akiwa na Mipira 2 ya Mabao / Assist 6).

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255657226571

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Cavion Nassir posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Contact The Business

Send a message to Cavion Nassir:

Shortcuts

Share

Category