Kagaba Media

Call

Kagaba Media HABARI ZOTE NA MICHEZO NA BURUDANI, KITAIFA NA KIMATAIFA UTAZIPATA HAPA πŸ‘

(USIKAE KINYONGE)

Vikosi vya Leo Simba vs namungo fc
02/11/2026

Vikosi vya Leo Simba vs namungo fc

Inaripotiwa kuwa Alejandro Balde hafurahishwi na namna suala lake lilivyoshughulikiwa.Watu wa karibu na mchezaji huyo wa...
02/11/2026

Inaripotiwa kuwa Alejandro Balde hafurahishwi na namna suala lake lilivyoshughulikiwa.

Watu wa karibu na mchezaji huyo wanahisi kuwa mawasiliano yote kutoka kwa Hansi Flick yamekuwa yakitolewa kupitia mikutano na waandishi wa habari badala ya mazungumzo ya moja kwa moja.

Balde alitarajia kocha huyo angezungumza naye binafsi na kumweleza mambo kwa uwazi zaidi.

Huenda Gavi anapitia moja ya nyakati ngumu zaidi katika maisha yake ya soka. Tangu kuanza kwa msimu huu, ameanza kwenye ...
02/11/2026

Huenda Gavi anapitia moja ya nyakati ngumu zaidi katika maisha yake ya soka. Tangu kuanza kwa msimu huu, ameanza kwenye kikosi cha kwanza katika mechi mbili pekee.

Kwa sasa, Gavi anahitaji kuonyesha uwezo wake kupitia vitendo zaidi kuliko maneno.

Mechi zijazo zitakuwa muhimu katika kubaini mipango ya Hansi Flick pamoja na nafasi na jukumu la mwisho ambalo Gavi atakuwa nalo ndani ya kikosi cha Barcelona msimu huu.

🚨 π‰πŽπ’π„Μ πŒπŽπ”π‘πˆππ‡πŽ πŸ‡΅πŸ‡ΉπŸ—£οΈ JosΓ© Mourinho: β€œImepita miezi 4, ambao si muda mrefu sana, na taratibu tunaendelea kufanya vizuri ...
02/11/2026

🚨 π‰πŽπ’π„Μ πŒπŽπ”π‘πˆππ‡πŽ πŸ‡΅πŸ‡Ή

πŸ—£οΈ JosΓ© Mourinho: β€œImepita miezi 4, ambao si muda mrefu sana, na taratibu tunaendelea kufanya vizuri zaidi. Kuna mambo ambayo sasa nimeyaelewa, ambayo sikuwa nimeyaelewa siku yangu ya kwanza.”

Al Ahly wanatarajiwa kuendelea kumuunga mkono Hussein Ammouta, lakini mchezo ujao dhidi ya Pyramids FC unaweza kuwa na u...
02/11/2026

Al Ahly wanatarajiwa kuendelea kumuunga mkono Hussein Ammouta, lakini mchezo ujao dhidi ya Pyramids FC unaweza kuwa na uzito mkubwa kuhusu mustakabali wake ndani ya klabu hiyo.

Kipigo katika mchezo huo kitaibua maswali zaidi kuhusu nafasi yake pamoja na mwelekeo wa timu.

"Mechi yetu na Mashujaa ndiyo mechi ya mwisho Yanga kuteseka. Tofauti ni alama 5, alama 3 wanazo Simba SC tukirudiana na...
02/11/2026

"Mechi yetu na Mashujaa ndiyo mechi ya mwisho Yanga kuteseka. Tofauti ni alama 5, alama 3 wanazo Simba SC tukirudiana nao mwezi wa pili. Alama moja iko upande wa mwenyekiti, alama moja iliyobaki iko upande wa mwekezaji [Simba SC]. Kabla ya uchaguzi Januari [wa Simba SC], Yanga atakuwa juu ya kilele cha msimamo." - Ally Kamwe, Afisa Habari Yanga SC

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Wa...
02/11/2026

Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi anamwakilisha Rais Samia Suluhu Hassan kwenye ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Wanawake wa Jukwaa la Mabunge la Ukanda wa Maziwa Makuu (ICGLR), unaofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) Dar es Salaam.

ARSENAL imevunja mwiko wa kutopata ushindi ndani ya miaka 14 kwenye Uwanja wa Anfield baada ya jana Novemba 1, 2026 kuic...
02/11/2026

ARSENAL imevunja mwiko wa kutopata ushindi ndani ya miaka 14 kwenye Uwanja wa Anfield baada ya jana Novemba 1, 2026 kuichapa Liverpool bao 1-0 katika mchezo wa Ligi Kuu England uliopigwa uwanjani hapo.

Shujaa wa Arsenal katika mchezo huo alikuwa mshambuliaji Kai Havertz, aliyefunga bao pekee dakika ya 16 akimalizia krosi ya kiungo Declan Rice.

Bao hilo lilitokana na makosa ya kipa wa Liverpool, Alisson Becker, ambaye pasi yake ilinaswa na wachezaji wa Arsenal kabla ya timu hiyo kufanya shambulizi la haraka lililozaa matunda.

Ushindi huo una maana kubwa kwa kikosi cha kocha Mikel Arteta, kwani ni mara ya kwanza kwa Arsenal kuibuka na ushindi wa Ligi Kuu England kwenye Uwanja wa Anfield tangu ilipofanya hivyo mwaka 2012. Wakati huo Arteta alikuwa akicheza nafasi ya kiungo chini ya kocha Arsene Wenger.

Matokeo hayo yameifanya Arsenal kufikisha pointi 24 baada ya michezo tisa na kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi tatu dhidi ya Manchester City inayoshika nafasi ya pili.

β€Ž

Kiungo mshambuliaji Emam Ashour ameendelea kusugua benchi katika mechi tatu mfululizo za Al Ahly.Ashour alianza kuwekwa ...
02/11/2026

Kiungo mshambuliaji Emam Ashour ameendelea kusugua benchi katika mechi tatu mfululizo za Al Ahly.

Ashour alianza kuwekwa benchi katika mechi ya mkondo wa pili ya raundi ya pili ya Kombe la Shirikisho barani Afrika (CAFCC) dhidi ya Kitara FC ya Uganda, mnamo Oktoba 25, 2026.

Mechi nyingine alizokosa ni ile ya Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Modern Sport FC iliyopigwa Oktoba 29, 2026, pamoja na mchezo dhidi ya Arab Contractors FC, ambapo kiungo huyo sasa anatimiza jumla ya mechi tatu nje ya uwanja.

Uamuzi wa kuwekwa benchi kwa kiungo huyo ulichukuliwa na kocha mkuu wa Al Ahly, Hussein Ammouta, kufuatia kutoridhishwa na kiwango cha Ashour wakati wa mechi ya Ligi Kuu ya Misri dhidi ya Al Qanah iliyomalizika kwa sare ya mabao 3-3.

Kocha mkuu wa KMC FC, Mohamed Muya, ana rekodi ya kipekee katika mechi nane za Ligi ya Championship zilizochezwa hadi sa...
02/11/2026

Kocha mkuu wa KMC FC, Mohamed Muya, ana rekodi ya kipekee katika mechi nane za Ligi ya Championship zilizochezwa hadi sasa.

Mtaalamu huyu aliyewahi kuzinoa timu za Fountain Gate na Coastal Union zilizopo Ligi Kuu, bado hajapoteza mchezo wowote akiwa na kikosi chake kipya kinachopambana kurejea daraja la juu msimu ujao.

Hadi sasa, Muya amekiongoza kikosi hicho kushinda mechi tano na kupata sare tatu, na kujihakikishia kuwa kocha pekee asiyeshindika kwenye ligi hiyo.

Mechi nane ilizocheza KMC FC
KMC FC 5-1 Mbuni FC
Bigman FC 1-3 KMC FC
KMC FC 3-0 KenGold FC
Bandari TZ 1-1 KMC FC
KMC FC 1-1 Gunners FC
Transit Camp 1-2 KMC FC
KMC FC 0-0 IAA SC
KMC FC 1-0 Stand United

USHINDI-5
SARE-3

β€Ž

Address

Dar Es Salaam

Telephone

+255745260055

Website

Alerts

Be the first to know and let us send you an email when Kagaba Media posts news and promotions. Your email address will not be used for any other purpose, and you can unsubscribe at any time.

Shortcuts

Share