04/09/2026
Mwekezaji wa klabu ya Simba SC, Mo Dewji, ambaye ndiye k**a rais wa klabu, amesema machache baada ya mahojiano na Madam Rita. Moja ya maneno yake alisema kwamba, “Klabu ya Simba SC bado muda tu niondoke. Kwanza niliomba klabu kwamba wanipe asilimia kadhaa ili klabu hii niweze kuitengeneza vizuri, lakini waliona k**a nahitaji pesa zao. Nilihitaji niwekeze pesa nyingi sana, lakini naona timu hii inaenda kuanguka kabisa na sitapata kitu.
Kuna vilabu vikubwa hapa Tanzania vimeanza kufanya vizuri, mfano mzuri ni Azam FC. Hii timu itakuja kuwa bora zaidi kuliko Simba SC. Nasema hivyo, namanisha kwanza wamejiweka sana, hakuna siasa kwenye mpira wao. Klabu yao haina ujanja ujanja, wanaenda k**a rula. Kwa hiyo k**a Simba SC inahitaji kupata mwenendo mzuri, waache siasa kabisa. Ndio maana nikasema kuna klabu zingine hapa zitakuja kuwa kubwa sana Tanzania na zitazidi hizi Yanga SC na Simba SC.
Barcelona, Real Madrid, Chelsea, Zamalek. Timu zote hizo zina wazamini wakubwa sana na pia wanafanya makubwa sana. Pia wanawekeza pesa nyingi mno. Kwa hiyo kuweka pesa nyingi ndio mwanzo wa mafanikio makubwa sana ndani ya klabu. Sasa kwa upande wangu mimi siwezi kuwekeza pesa nyingi sehemu ambayo haina mapato. Nimeisaidia timu ili kuweka ukubwa wa ligi. Nasema naipenda Simba SC tu, ila k**a ningekuwa sina lengo na timu, ningeiacha.
Naomba Wanasimba SC waache siasa kabisa kwenye timu yangu. Mimi nasema hivyo naumia sana kuliko wanavyozani. Na k**a nikisema niiachie klabu hii, basi inaweza kufanya vibaya zaidi. Ndio maana kila kitu nafanya ili kulinda jina la Simba SC pamoja na viongozi wa klabu, mashabiki pia. Nimetumia mabilioni ya pesa ili Simba SC ikuwe, pia nikaweka history kubwa kule kwa wenzetu Waarabu.” . . . .