29/08/2026
Paris Saint-Germain ilishusha bei yake ya awali ya £145 milioni hadi £123 milioni kwa ajili ya kumuuza Bradley Barcola.
🇫🇷 PSG ilisisitiza kupata kiasi kikubwa zaidi ya fedha zilizolipwa kwa Morgan Rogers (£117M) na Elliot Anderson (£116M).
Pia, mabingwa hao wa Ufaransa walilenga kuvuka thamani ya dili lililompeleka Yan Diomande kwenda Real Madrid.
Kwa sasa, PSG imekusanya karibu £340M+ kupitia mauzo ya wachezaji ambao hawapo tena kwenye mipango ya klabu.
🔴 Liverpool na Barcola wako kwenye hatua za mwisho za kukamilisha dili hilo, ambalo linaweza kufikia £123 milioni pamoja na nyongeza.
📰 Chanzo: Ben Jacobs