29/08/2026
T.M.A imetoa tahadhari ya mvua za El Niño za mwezi October mwaka huu, ni vyema ila wasiwasi wetu ni kuwaandaa kwa naneno kunatosha?. Tunajiuliza Mito na Makorongo iliyopoteza mwelekeo ineandaliwaje. Watu waliojiimarisha kwenye mikondo ya maji wamepewa elimu kiasi gani ili wahame kwa hiari kujisalimisha? Tunajifunza kwa kiasi gani kutokana na yanayotokea kwa wenzetu? Ramani ya asili ya nchi nani anayo kutambua Mito iliwahi kupita maeneo gani kabla ya kukauka na kuwa tambarare iliyowavutia watu Kujenga? Ikiamua kurudi hiyo Mito kwenye mikondo yake, waliojenga katika maeneo hayo wamejiandaaje kusalimika? Haya ndiyo maswali tunayoendelea kujiuliza muda huu, tukifuatilia yanayotokea kwa wenzetu.