31/05/2021
TUKISEMA UKWELI ETI TUNAONGEA SANA.
Follow MANJA SPORT news
Nilishawahi kuandika hapa kwamba Yanga inahitaji uongozi bora au viongozi waliopo wakasome Qualities of good leadership,k**a wanajua Qualities za kiongozi basi wamesahau wakumbushwe,Kama hawajasahau basi waiache Yanga maana wanaiharibu Brand ya Yanga kwa makusudi.Nikaambulia kutukanwa.
Nilisema hayo baada ya kupata taarifa kwamba Carlinhos anajiamulia mambo ya kufanya na viongozi wakawa wanamtetea,Carlinhos alikuwa hataki kulala na wachezaji wenzie kambini alikuwa anataka kulala peke Yake.Viongozi wakamkingia kifua.
NILIKUWA NAWAKUMBUSHA TU EMBU TUENDELEE....
Hili la Carlinhos badala ya watu wa timu fulani kucheka na kufurahia tuchukue k**a Somo,kwani hii haijatokea kwa Yanga tu.Simba walikuwa na Junior Lukosa na Peter Mduhwa hawa waliishia kuvaa jezi tu.Azam walikuwa na Thierry Akono akaishia kuwa mtalii wa miezi kadhaa na kusepa.
Kwanini haya Yanatokea? Kifupi ni kwamba yanatokea kwa sababu timu zetu hazitumii Scouting kufanya sajili zao.Kifupi wakiona tu jamaa mweupe au mtu aliwahi kufunga magoli 17 na Esperance wanasajili.Nimesahau au wakiona ana Rasta.
Timu zetu zingekuwa zinatumia Scouts kufanya Sajili Yanga wangeijua tabia ya Carlinhos mapema sana hivyo wasingemsajili au wangemsajili na wangejua namna ya kuishi na Carlinhos.
Namaliza kwa kusema Africa ni africa,yaani mtu k**a carlinhos anaachana na klabu kwa sababu za kitoto kabisa.Eti kwa sababu ya mapenzi.Japo kunaweza kuwa na sababu nyingine ila na mapenzi ni moja ya sababu,yaani anataka kuwa karibu na mke wake.
follow hussein manja,