05/08/2021
✍️... EPL🏴 REMINDER⚽
LEICESTER CITY-PART 2.....INAENDELEA;
Baada ya kufanikiwa kusalia kwenye ligi kuu, Nigel Pearson akaachishwa kazi Kwa matamshi yake ndani ya press conference Kwa kumtukana mwandishi wa habari....' and I.. think you are an ostrich 😂,' ndio matamshi yaliomwachisha kazi kocha huyu. Kibarua kikawa kumtafuta meneja wa kumrithi.
Mara jina likatokea; Claudio Ranieri- washika dau wa soka wakashangaa Sana na uamuzi huu, moja wao akiwa Gary Linker. Lakini msimamo wa mabosi wa Leicester City ukawa ndio huo, Claudio Ranieri ndiye haswa😃.
Msimu wake wa Kwanza akiwa mkufunzi, hakuna aliyetabiri kuwa angefanikiwa na kilabu hiki cha East Midlands.
Mechi baada ya mechi... Wikendi baada ya wikendi... Goli baada la lingine... The Foxes wakaanza kutamba. Kila wikendi ungewasikia watangazaji wa soka wakitaja majina k**a👉 Jamie Vardy, Albrighton, Mahrez...yote kisa, maajabu walikuwa wakiyafanya uwanjani..ukawa ni mwendo wa pointi tatu kila wikendi. Mashabiki wakaaanza kuamini kuna Jambo la kutokea😃....
Hata inapofika Januari mwaka wa 2016 Leicester City ndio walikuwa kileleni, wakawa k**a ndovu aliepanda mtini hakuna ajuawe alivyofika pale😅...
Mechi moja nusura iwapokonye roho mashabiki wa Leicester city 😂.... February Ile Danny Welbeck anazamisha free kick yake Ozil kwenye wavu wa Shmichael, wakajua kombe limewatoka vile, kumbe ya Mungu mengi tu 😁....
Wapinzani wao wa karibu Spurs wakawa na mechi ya MUST WIN dhidi ya Chelsea kuzuia kombe lisiende King Power stadium. Mashabiki wote wa Leicester City, ikiwemo Mimi😂 tulikuwa kwenye banda umiza😂😂 tupo nyuma ya Chelsea . Ila kipindi cha Kwanza kinakamilika; Chelsea 0-2 Spurs.Duh🙆♂️...tukajua hapa pagumu....
Kipindi cha pili Cahili pamoja na Eden Hazard wakahakikisha Spurs wanapoteza alama mbili na kupeleka ubingwa 🏆wa kihistoria King Power statdium...
Ukawa ndio ubingwa 🏆Bora wa muda kuwahi kushuhudiwa EPL...hivi kutatokea surprise nyingine msimu mwingine 🤔au ndio hivo?
Tbt hiyo👇