02/09/2026
🇰🇪MANSLAUGHTER (Kuua bila nia ya kuua)
Siku moja huko Mumias, Bwana Nyang'au na jirani yake waligombania mpaka wa shamba. Hasira zikapanda, wakaanza kupigana kwa ngumi. Nyang'au akamsukuma mwenzake, akaanguka vibaya na kupiga kichwa kwenye jiwe. Baadaye akiwa hospitalini, yule jirani akafariki.
Je, hii ni murder?
Jibu: Si lazima. Mahakama inaweza kuamua kuwa ni manslaughter ikiwa kifo kilitokana na kitendo kisicho halali lakini bila kuthibitishwa kuwa kulikuwa na malice aforethought (nia ya kuua).
📖 Sheria: Kifungu cha 202 cha Penal Code.
⚖️ Adhabu: Kifungu cha 205 kinasema mtu anayepatikana na hatia ya manslaughter anaweza kuhukumiwa kifungo cha maisha.
🧠 Kumbuka: Tofauti kubwa kati ya murder na manslaughter mara nyingi ni nia ya kuua na mazingira ya tukio.
💬 Swali: Unadhani ugomvi wa dakika 5 unaweza kuharibu maisha ya familia mbili milele?