31/08/2026
Kwa miaka mingi, wananchi wamekuwa wakilia kuhusu maendeleo, matumizi ya fedha za umma na uwajibikaji. Lakini swali limeendelea kubaki: Seneta wetu alikuwa wapi wakati mwananchi wa Kilifi alihitaji sauti yake? Oversight ilikuwa wapi?
Ni kweli, Seneta si wa kuleta misaada. Lakini yeye ndiye sauti ya wananchi, mlinzi wa ugatuzi na msimamizi wa Serikali ya Kaunti. Kazi yake ni kuhakikisha viongozi wanawajibika na kila shilingi ya mwananchi inalindwa.
Leo, baada ya Wakili Hon. George Kithi ,kuamka na Kilifi kuonyesha wazi kwamba inataka mageuzi, ghafla tunaona viongozi k**a senator Hon. Stewart Madzayo,EGH,MP. wakikimbia kutoka Nairobi kila weekend kuja Kilifi! π₯
Swali ni moja: Mlikuwa wapi miaka yote hiyo?
Kilifi ilipokuwa na changamoto, sauti zenu zilikuwa wapi? Wananchi walipokuwa wakilia kuhusu maendeleo, mlisimama upande gani?
Lakini sasa mambo yamebadilika. Wananchi wameamka! Hawataki tena viongozi wa kusubiri uchaguzi ukaribie ndipo waonekane.
Wanataka uwajibikaji. Maendeleo. Usimamizi wa fedha za umma. Na sauti ya kweli katika Seneti.
πͺοΈπ₯ UPEPO WA KILIFI UMEBADILIKA!
KILIFI IMEAMUA!
2027 tunataka Seneta mwenye uelewa wa sheria, uwezo wa kusimamia Serikali ya Kaunti na ujasiri wa kusimama bila woga kutetea mwananchi.
WAKILI Hon. George Kithi NDIYE CHAGUO LA MAGEUZI! βπ₯
KITHI APEWE KITI β NA HADHI YA KILIFI ISONGE MBELE! π°πͺπ₯
Akida Kilifi