12/05/2021
.... LIPO TUMAINI, THERE'S HOPE! Ayubu 14:7-8,
Kwa maana lipo tumaini kwa mti, k**a ukikatwa utachipuka tena, nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. Mizizi yake yaweza kuchakaa ardhini
na kisiki chake kufa udongoni, lakini kwa kupata dalili ya maji utachipua na kutoa machipukizi k**a mche...at least there is hope for a tree if it is cut down, it will sprout again, and it's new shoots will not fail.....mti unaweza ukakatwa na habari njema ni kwamba huo mti utachipuka tena, kwa harufu ya maji huu mti utapata uhai na utasimama tena nayo machipukizi yake mapya hayatakoma. Unaweza kuwa umekatwa na hauna nguvu ya kusimama tena, lakini kwa kusikia neno hili utasimama tena. Kuna machipukizi mapya yanayochipuka katika maisha yako, haya machipukizi hayatakoma, yatachipuka na kufanya usimame tena. Be encouraged kwamba hapo ulipo si mwisho wako, biashara kuanguka, ndoa kuharibika, kupoteza kazi na mengi sio mwisho, utasimama tena! Barikiwa sana na Tukutane Galilaya! MAMA TAIFA EVAH Mwalili